Ni ujumbe unaotokea kwenye simu yangu kila napojaribu kufungua app ya camera, ni simu aina ya blackberry Q5. Wakati wote nimekuwa nikitumia line ya voda, kabla tatizo hili halijaanza siku 2 zilizopita niliweka line ya halotel kwa muda fulani..sijui kama hii ndiyo yawezakuwa sababu lakini hata baada ya kurejesha line ya voda na ku-restart simu mara kadhaa camera inagoma kufunguka. Naombeni msaada wazoefu, nifanye nini. Natanguliza shukrani