The Bottom line ya sanaa ya kutongoza


KIPAJI YA KUZALIWA HIYO...HAIFUNDISHWI...:wink2:
 
Aisee we mkali..
Asante kwa dondoo..
 
Ndio tatizo la watanzania wengi, hasa viongozi wetu wa nchi ndio maana tunaletewa mpaka wamachinga wa kichina na wapaka rangi wazungu. Sitaki niongee sana, lakin ukifanya kitu kizuri, ni ngumu sana mtanzania mwenzako akuamini

Hapo umenena mkuu, na tukiendelea hivi tutaletewa hadi wachanganya zege wa kigeni
 
mmmhhhh umetoa siri zangu Miss Judith,sasa mimi ninamtongozaje CPU? thanks,good analysis!!
 
what you have written can be 8 paragraphs but the content weights more than 8000 paragraphs
 
Bonge la tutorial,...mwah mwah ntasoma baadae lakini
 
sijatilia mashaka uwezo wake SMU, yawezekana anao uwezolakini kwa nature ya kazi inaonesha kabisa kuwa vingi si vya calture zetu! tumeshuudia watu wengi wakipata umaarufu kutafsiri kazi za wenzao, mfano ni E. Shigongo!

Duh! Mbona unatilia shaka uwezo wake?
 

(kwenye red)hadithi yako nzuri sana mkubwa!(btn ze linez!!)
 
thanks kwa ujumbe bomba,watanikoma kitaa sasa.
 
Nakubaliana na mwandishi wa thread lakini mbinu za kutongoza zinatofautiana kulingana na ulinzi wa hilo gereza. Magereza mengine yana walinzi wenye silaha kali lakini wakisomeshwa kidogo tu, wanalainika na kuruhusu wezi kuingia gerezani. Kwa mfano ukienda kwa wa wahaya hakikisha una akiba ya senene mfukoni ili unapo-sign-off unamwachia bibie anakula wakati anatafakari 'paper' uliyopresent.
 
KAMA KUTAKUWA NA UFISADI WA AINA HII NI MZURI SANA NA HATA JINA LA UFISADI LITAPOTEA, MAANA AMEFICHUA SIRI NZITO,
mimi nilkuwa najua sana maana nimeshatongozwa mara nyingi bila ya kujua. Hongera Judy kwa kutupa mambo
JUDY article yako ni nzuri sana na ya kuvutia, hongera sana! ILA NINA MASHAKA KUWA HIYO KAZI SIYO YAKO, EBU JARIBU KU ACKNOWLEDGE ORIGINAL SOURCE YA HIYO KAZI! KUTOKUFANYA HIVO NI WIZI MKUBWA SAWA NA UFISADI NDANI YA UAKADEMIA!
 
Hiyo nayo sawa lakini kumbinya kiganya si kwa mtu humjui kabisaaa, inakkuwa ni mtu ambaye unamjua ila yeye haoneshi kama anakupenda, ivo wewe unamuwahi kumwambia ili asiende kwa wengine.
 
Usikatae ukweli, Huyu Judy yupo right 99.9% na sema tu kuwa mengine kaacha kama alivyo sema. Mbinu ni nyingi ila ujumbe mkuu ndo huo
asante Miss Judith 75 % inaweza kuwa kweli
 
Hiyo kutongoza kwa mwanamke nilikuwa naita 'kujilengesha' au 'kutega'. Kumbe twatongozwa sana tu eeh?
 
Ni ukweli uliowazi nakupa 85% kwa ujasiri wako wa kutohoa mada ngumu hasa katika utekelezaji wake
 
jamani mnisamehe nilikuwa bize sana nikashindwa kujibu hoja zenu, lakini nashukuru kuwa wengi wenu menielewa na lengo langu lilikuwa ni kushea tu uzoefu wangu na maandoshi yangu haya ni yangu mwenyewe, sijayanakili wala kuyanukuu toka mahali popote.

nakubaliana na aliyesema kuwa japo kuna para 8 tu mambo yaliyomo huenda yangehitaji para zaidi ya 8000. ni kweli kama mtakavyoona hata mbinu zenyewe sikuweza kuzifafanua vizuri moja baada ya nyingine, sasa kama ningefafanua kwa undani, sijui ningeandika kitabu kikubwa kiasi gani!

kutongoza kwaweza kuwa na mitazamo kadha wa kadha ila kutongoza si kitu kibaya na nimekiri kuwa hata mie nilishatongoza mara nyingi. lengo ni kupanua mawasiliano na hata kutaongeza marafiki na pengine wachumba na hata wake/waume watarajiwa. sanaa hii ya kutongoza ikitumiwa vizuri italeta furaha maishani mwa mtu kwani huleta marafiki karibu na kumfanya mtu ajisikie kuwa kati ya jamii na kuondoa upweke. ikitumiwa vibaya, huharibu sifa ya mtu na kumfanya aonekane malaya/mhuni, nk

wanawake na wasichana wanapaswa kutoona haya kutongoza ila wawe makini wasijeonekana vituko kwani jamii yetu bado ina mitazamo isiyo sawa kwa wanawake na wanaume juu ya kutongoza. si lazima msichana akimtongoza mtu basi wamalizie na ngono, wanaweza kupanga hilo baadaye kadiri itakavyoonekana inafaa lakini pia wanaweza kishia kuwa marafiki wa kawaida tu.

nlipokuwwa kidato cha pili nliwahi kumtongoza mvulana fulani na siku moja ya jumamosi ambayo haikuwa siku ya shule (kwa tuliosoma day school) nikamfuata kwao na kumtaka twende tukaongee mambo yetu shuleni manake nilikuwa napenda sana maongezi yake. kwa kweli kuanzia siku iyo alinisumbua sana akitaka tufanye ngono nami nikabaki njia panda. ngono sitaki kufanya na kumuudhi sitaki, nataka aendelee kuwa rafiki yangu. mwishoni hatimaye alinielewa laini alikuwa na huzuni siku zote na hakuwa akinifurahia tena hadi tunaachana baada ya kumaliza form four. so mtaona hatari ya msichana kutongoza.

i hope mtanielewa na nawatakia kila la heri wote wanaotongoza ama kutongozwa.

stay blessed
 
Kwa hizi mbinu za mwanamke, sasa naanza kuamini nimetongozwa zaidi kuliko nilivyotongoza

we acha tu........mimi nilipokuwa chuo kuna mdada alikuwa anapenda sana kunitkea room....tatizo mshkaji wangu alishapita....nikaona nikipita dizaini itakuwa sio fresh.....ila kitu ya haja
 
Sijawahi kutongoza, ngoja nijaribu.
Ahsante miss jud kwa maujanja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…