Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
#ALHAMISI kama ya leo miaka zaidi ya 2000 iliyopita Yuda (Iskariot) mmoja wa wale Thenashara, alimsaliti BWANA Yesu. Akamuuza kwa wayahudi kwa vipande 30 vya fedha na kesho yake Yesu akauawa. #TheBlackThursday.!
#ALHAMISI kama ya Leo tarehe 26, April mwaka 1945 kiongozi wa Ujerumani Adolph Hittler alideclare kukata tamaa ktk mapigano ya vita vya pili vya dunia. Majeshi ya adui yalizidi kumsogelea kabla ya kuamua kujiua mwenyewe April 30, 1945. #TheBlackThursday
#ALHAMISI kama ya leo tarehe 24, October mwaka 1929, dunia ilishuhudia mdororo mbaya zaidi wa kiuchumi kuwahi kutokea. Maduka ya hisa yalifungwa, mabenki yakafilisika, bidhaa zikaozea maghalani. #TheBlackThursday
#ALHAMISI kama ya leo tarehe 11, June mwaka 1962, Nelson Mandela alihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa mashtaka ya uchochezi. Upande wa mashtaka uliomba apewe adhabu ya kifo lakini Jaji akamhukumu kifungo cha maisha, lakini akatumikia miaka 27 kabla ya kiachiwa huru. #TheBlackThursday.!
#ALHAMISI kama ya leo tarehe 14, October mwaka 1999 Mwal.Julius Nyerere alifariki dunia huko hospitali ya St.Thomas Uingereza kwa kile kilichoelezwa kuwa ni "saratani ya damu". Tanzania ikampoteza baba wa Taifa. #TheBlackThursday.!
#ALHAMISI ya leo, June 30 mwaka 2016 mbunge wa Singida Mashariki Mhe.Tundu Lissu anapandishwa mahakamani kwa madai ya kutoa kauli za uchochezi (Just like Mandela). #TheBlackThursday.!
#ALHAMISI ya leo, June 30 mwaka 2016 wabunge wa UKAWA wanaandamana kutoka bungeni wakiwa wamevalia mavazi meusi kama ishara ya maombolezo, kupinga serikali kuongoza nchi "kidikteta" #TheBlackThursday
#ALHAMISI ya leo June 30 mwaka 2016, Tanzania inashuhudia siku ya mwisho ya unafuu wa maisha kwa mwananchi maskini. Kuanzia kesho July 1 maisha yatakua magumu isivyotarajiwa.Gharama za kutuma na kupokea pesa zitaongezeka maradufu, bei za bidhaa zitapanda, thamani ya shilingi itazidi kuporomoka etc. Wakati hayo yakitokea kutakuwa hakuna nyongeza ya mishahara, wala kupandishwa vyeo, wala ajira mpya serikalini. #TheBlackThursday.
Kwa kawaida inapofikia hali hii watu wengi waoga huamua kuungana na "tabaka tawala" ili kujipendekeza kwa kudhani watapata unafuu wa maisha ama vyeo. Ukisema hakuna sababu ya serikali kupandisha gharama za bidhaa watasema ni wajibu wa wananchi kulipa kodi. Lakini wanasahau kwamba kinachopingwa sio wananchi kulipa kodi, kinachopingwa ni kiwango kikubwa cha kodi kwa mwananchi mnyonge.
Kuanzia kesho mwananchi maskini ataanza kutozwa 28% ya gharama za kutuma na kupokea fedha kwa njia ya simu (18% VAT, &10 sehemu ya faida). Note; sio 28% ya fedha unayotuma, ni 28% ya gharama za makato. Lakini wakati wananchi maskini wakikamuliwa 28% makampuni ya madini yanalipa mrabaha wa 04% tu. Ukihoji utaitwa mchochezi. #TheBlackThursday
Ni watu wachache sana wanaoweza kusimama kidete na kuhoji kwa maslahi ya umma bila woga wala upendeleo. Wengi watahofu, na wengine watataka kukuadhibu wakiona unahoji, watakukosoa kuona unasema ukweli, kwa sababu wamezoea kujipendekeza. Usiogope kwa kusema ukweli. Ukweli hauwezi kubadilika hata kama utasemwa na mtu mmoja.
Rais wa kwanza wa India Mahatma Ghandi aliwahi kusema "Many people, especially ignorant people will need to punish you for speaking the truth, for being you. Never apologize for being correct. If you are right and you know it, speak your mind. Even if you are a minority, or one, the truth is still the truth."
Kwa tafsiri isiyo rasmi Ghandi alimaanisha, watu wengi (hasa wajinga) watataka kukuadhibu kwa kusema ukweli. Usiombe radhi kwa kuwa mkweli, usijutie kwa kwa kuwa sahihi. Kama unajua ukweli usiogope kusema. Ukweli utabaki kuwa ukweli hata kama unasemwa na wachache.
Ukweli mmoja wapo ni kwamba sioni Tanzania yenye neema inayohubiriwa na wanasiasa. Siamini kama Tnzania ya viwanda itajengwa kwa kukamua maskini na kuacha makampuni ya kigeni kufaidi rasilimali zetu kama madini na gesi. Siamini kama maendeleo ya kiuchumi yataletwa kwa kutegemea kupandisha ushuru wa pombe na sigara. Siamini hivyo, unless kama tutachange approach.
Tushauri serikali iwe na njia mbadala zenye tija katika kuleta maendeleo badala ya kumuumiza maskini. Mwalimu Nyerere aliwahi kukemea serikali kukimbizana na maskini barabarani kuwakamua kodi lakini ikaacha kutoza kodi kwa matajiri wanaoinyonya nchi. Tuikosoe serikali, tuishauri njia mbadala, tuseme ukweli kwa faida ya mama Tanzania. Tusiogope kusema ukweli hata kama dunia nzima itakuwa kinyume na sisi.
Alhamisi ya June 30, mwaka 2016. Alhamisi mbaya zaidi kwa mwaka huu, alhamisi nyeusi, alhamisi ngumu, alhamisi ya "kifo cha demokrasia", alhamisi ya "kifo cha maisha bora" Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru. #TheBlackThursday.!
Malisa G.J