Thamani ya mzazi baada ya kuanza mapenzi

Thamani ya mzazi baada ya kuanza mapenzi

KOROE

Member
Joined
Dec 6, 2017
Posts
90
Reaction score
770
Natumaini wazima,

Hakuna kama wazazi, wao pekee ndo wenye upendo wa dhati kwetu, wao ndo watu wa mwisho kabisa kusimama nasi tunapopita kwenye matatizo baada ya wote kutukimbia, upendo wao hauna sababu, ndani ya moyo wao wanatupenda, hata tukiwaje wao wanatupenda.

Mikiki mikiki ya mapenzi sometimes inatufanya tusahau jukumu letu la kuwalea, ni rahisi sana kumpa mpenzi laki moja wakati wa sikukuu wakati mama au baba yako umemtumia elfu 30 maajabu ya hawa wazazi wetu huwa na moyo wa shukurani sana hata kwa kitu kidogo kuliko hata wapenzi wetu,

Hata tunapokuwa na wapenzi, jamani tusisahau kuwa kuna wazazi nao pia wanatuhitaji.

Kila mtu ajiulize sikukuu hii amapenga kumfanyia nini mpenzi wake na amepanga kumafanyia nini mzazi wake.. WAZAZI PIA WANATUHITAJI.......TUWALINDE, TUWALEE, TUWATHAMINI.

Nimeona tukumbushane kidogo.

Siku njema
 
Nashukuru nimejifunza katika Uzi wako narekebisha pale nilipokosea mungu anitie nguvu
 
Thank you bro for good message sure I like it!!!!!!!they took care of us since we are children √√√√
 
Nashukuru kuona kizazi chenye akili,huruma na moyo wa dhat kwa wazazi bado kipo..mungu akulinde na tuwapende wazazi kwani pepo ya dunia ni mama na baba
 
Back
Top Bottom