Jokajeusi
JF-Expert Member
- Jun 1, 2018
- 6,332
- 10,913
Murevedi vose!!
Moja kwa moja kwenye Mada.
Mwanamke anathamani kuliko kiumbe chochote hapa duniani. Kwa kulitambua hili sisi kama wanaume tuliopewa dhamana ya kuiongoza hii dunia tumejikuta tukiwaheshimu na kuwatunza wanawake zetu.
Kila unayemuona hapa duniani ameletwa na mwanamke. Manabii wakubwa wote walizaliwa na wanawake, majemadari na watu wote mashuhuri.
Ili kitu chchote kiwe na thamani lazima kiwe adimu. Hiyo ndiyo sifa ya kwanza. Mwanamke zamani alifichwa ndani, hakuruhusiwa kuonekana hovyo hovyo akizurura bila msingi wowote. Hii ilifanya wanawake wapewa heshima kubwa. Wanwake walijisitiri haswa. Na kwa jamii za waafrika ambao hatukuwa na mavazi basi mwanamke alikuwa anafichwa ndani. Jambo hili halikufanyika kwa bahati. Hata baadhi ya dini zinaonyesha jambo hili.
Kiutaratibu si halali wanawake kukaa vibarazani kunako njia wakipiga soga wakati wanaume wakipita na kuwatolea macho.
Mzee wangu aliwahi kunambia siku nikioa basi mke wangu kila apatapo ujauzito na kujifungua basi ni mlipe pesa ndefu. Pia alinambia mwanamke akafanya kazi za nyumbani kama kufua, kupika na usafi basi napaswa kumlipa pesa kwa mwezi. Akimaanisha mwanamke hapaswi kufanya kazi yoyote isipokuwa kujiremba, kugegedwa na kuangalia watoto.
Lakini kinachotokea ni kuwa jinsi wanawake kutaka haki za wanaume na uhuru wa kutembea, kutafuta pesa na mambo mengine kama hayo ndivyo thamani yao inavyoshuka chini. Kwa sasa wanawake hawana thamani tena na tunapoelekea watazidi kudhalilika na kuzalilishwa.
Ona wanavyokaa uchi na kujipost mitandaoni. Ona wanavyotafuta wachumba na bado wanakosa. Ona wanavyoolewa bila ndoa wala harusi. Yote hii inaonyesha uthamani wa mwanamke umeshuka kwa kiasi kikubwa.
Uhuru wa mwanamke humdhalilisha mwanamke mwenyewe. Mwanamke ameumbwa kuangaliwa na kuchungwa kama mtoto. Asipochungwa huwa kama Chokoraa tuu. Ona wanawake wa siku hizi walivyo machokoraa. Kuzurura bila mpango. Mwanamke anatoka nyumbani eti kwenda kutembea bila msingi wowote, bila uangalizi wowote. Nao ndio wanapenda kwani hudhani ndio kuheshimiwa kumbe ni kudhalilika.
Wanawake wenye akili hujua kuwa kuzurura na kukaa uchi ni moja ya tabia za kichokoraa. Ukiona mme wako hakuulizi uvaapo uchi na uzururapo bila msingi wowote ujue hajui thamani yako. Kitu kizuri lazima kilindwe, kitunzwe na kifuatiliwe kila mara.
Kama wanawake wakijificha na kujihifadhi kama zamani huwezi sikia wanaume wakiwatukana wanawake. Huwezi ona mwanamke anayetafuta mwanaume wa kumuoa kwani wanaume watakufuata wenyewe.
Mwanamke mwenye thamani lazima aolewe kwa ndoa na mahari. Hii ni heshima kubwa kwa familia na mwanamke mwenyewe. Lakini ukiona jambo hilo halijatukia basi kuna walakini wa uthamani wa mwanamke husika. Mimi kama mwanaume naongea kuwakilisha wanaume wengi. Wanaume wataungana na mimi kuwa ikiwa mwanamke unamuelewa na unampenda suala la mahari halitakusumbua na wala suala la ndoa halitakusumbua. Wanaume wengi tunapenda kuoa hata kwa ndoa ya mkeka tukiwapata wanawake tuwapendao. Lakini kinachotokea ni kuwa mimi kama mimi naweza kuoa kufumba na kufumbua mwanamke yeyote bila hata mia. Hii ni dharau na uzalilishaji kwa kweli.
Mwanamke mwenye thamani hufanya kazi kwa bidii. Hata vitabu vya dini vinasema mwanamke mchapakazi huyo atasifiwa. Mwanamke licha ya kwamba niliambiwa na mzee wangu asifanye kazi na akifanya basi nimlipe lakini thamani ya mwanamke ni pamoja na kujishuhulisha. matokeo yake nyumba itakuwa safi, watoto watakula kwa wakati, mme na watoto watakuwa nadhifu, familia itakuwa na akiba n.k. Lakini kinachotokea kwa sasa usishangae mwanaumekavaa marapu rapu wakati anamke. Ukiona mwanaume wa hivyo jua anafua nguo mwenyewe na mke wake ni mchafu au hamuwezi.
Kwa leo niishie hapo ila kwa kukumbushia tuu ni kuwa, jinsi wanawake wanavyotaka kuwa huru ndivyo wanavyozidi kujizalilisha na thamani yao inazidi kushuka.
Nawasilisha