Thamani ya mke wako katika maisha iko hivi

Thamani ya mke wako katika maisha iko hivi

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,746
Reaction score
25,639




KUWA mwanaume si kigezo cha msingi cha kuwa na mke. Mke anahitaji mwanaume makini, mwenye kujitambua na kujua kutekeleza wajibu wake.


Mtu mwenye sifa hizi hawezi kuwa mwanaume yeyote. Ni lazima awe mwanaume maalum, mwenye maarifa, heshima na thamani.


Nimeona wanaume wengi wakishindwa kuwapa hadhi na heshima stahili wake zao. Kwa kuwa wanajua wake zao wako ndani wanachukulia kitendo hiko kama mtego uliowanasa hivyo hawana ujanja.


Kwa sababu hiyo basi wanaume wengi utakuta wanafanya usaliti na kuvunja heshima na thamani ya wake zao hata kwa watu wasio kuwa japo na nusu ya heshima na thamani zao.


Yote hayo wanayafanya kwa sababu wanajua wake zao wako ndani, hawawezi kuondoka na kila wanapowataka wanawapata. Kuna kitu wanaume hawa wanashindwa kukifahamu kwa kina.


Wanashindwa kujua vitendo vyao viovu ni mbegu itakayokuja kuvunja kabisa utulivu wa nyumba zao na kuwaacha wao wakijuta na kuumia. Kila mwanaume anapaswa kujua kuwa mke wake ni binadamu mwenye hadhi na thamani ya kipekee.


Mke wake ndio anaijua thamani na udhaifu wake. Mke wake ni muhamasishaji namba moja wa mafanikio ama kushindwa kwake. Hivyo kitendo cha mwanaume kumdharau mke wake eti kwa sababu ya vimada si tu ni dhambi mbele za Mungu ila pia ni kujenga mizizi ya kuharibu thamani na heshima ya nyumba yako.


Kumbuka vimada huwa wanakuwapo kipindi cha mavuno na mafanikio ila mke wako huwa nawe kipindi chote. Kumpotezea mke wako nyakati umepata si tu ni dhambi ila pia inamjengea hali ya chuki na hasira juu yako.


Katika familia moja nilikuta mume akiwa katika hali mbaya sana ya ugonjwa huku mke wake akiwa haonekani kumjali sana. Kila mmoja aliumizwa na kitendo kile nikiwemo mimi. Ila bahati nzuri nilifanikiwa kuongea na mke wa muhusika.


Ni mwanamke mwenye umri wa miaka 36, mama wa watoto wanne. Mwanamke yule alinihadithia historia ya ndoa yake na mumewe kwa urefu sana. Kwamba walianza zamani sana wote wakiwa vijana wadogo kabisa huku wakiwa hawana maisha ya uhakika.


Baada ya miaka kadhaa, walifanikiwa kujenga nyumba, kununua magari na kuwa na biashara kubwa. Kitendo cha kuwa na maisha ya uhakika, ghafla kikaondoa furaha katika nyumba yao. Mume hakuwa yule tena.


Alijipa u busy hata asiweze kukaa na familia yake. Kila siku zilikuwa safari zisizokuwa na kichwa wala miguu. Na kote huko alionekana akijivinjari na wasichana wa kila aina. Mke wake alipomuuliza, alifokewa na kupigwa.


Mwanamke husika alivumilia kwa kuamini ipo siku mumewe atabadilika. Ila hakubadilika. Kadri siku zilivyokuwa zikienda mbele hali ilikuwa mbaya sana kuliko ilivyokuwa jana.


Mume wake akafikia hatua hata ya kumletea wanawake ndani. Haikuishia hapo akadiriki hata kumnyima haki yake ya msingi katika ndoa kwa kebehi na dhihaka. Yote hayo yalikuwa yakimuumiza na kumtesa sana yule mwanamke.


Kila siku akawa mtu wa kulia na kulaumu. Uzito wake ukapungua na hata muonekano wake mzuri ukaharibika. Baada ya muda mrefu wa kuumia na kuteseka akaamua kwenda kwa mtaalamu wa saikolojia( sio mimi).


Akapata ushauri uliomuweka sawa na kuamua kusonga mbele huku akiachana na hisia zozote kuhusu mumewe. Miaka minne baadaye, mumewe akapata maradhi ya figo na ini.


Akiwa hoi kitandani mama watoto wake hakuonesha kujali wala kuthamini. Japo kipindi alipokuwa kiteswa na mumewe alipewa ushauri wa kumuweka sawa ila hakupewa tiba ya kufukia majeraha yalioachwa na mume wake katika nafsi yake.


Huo ni mfano mmoja. Ila iko mingi. Chochote unachomfanyia mwenzako leo, kesho kinaweza kuwa fimbo ama moto wa kukuunguza.


Mke wako ni faraja na raha pale unapokuwa mwenye heri na mapenzi kwake ila pia kama ukiwa tofauti naye kipindi anapokuhitaji sana tegemea maumivu makali ikifika kipindi cha wewe kumuhitaji.

credit: Gazeti La Bingwa tz
 
Mlioishi kwenye ndoa miaka 20 njooni mtupe uzoefu
 
Ujumbe mubashara Sana yani ni Kama umenisema Mimi daaaaaaaaaaahhhh
 
Huo ni upande mmoja, je vipi thamani ya mwanaume kwenye ndoa? Vipi mwanamke anapokengeuka?
 
Back
Top Bottom