Thabo Mbeki aunga mkono wapinzani wa Zuma

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Thabo Mbeki anawataka wabunge wa chama cha ANC kutenda yatakayowafaa raia na sio kile kitakachofaidi chama, wakati wa kujadili mswada wa kutokuwa na imani na rais Jacob Zuma, wiki ijayo.

Wito wa Mbeki huenda ukawakera wanaomuunga mkono Zuma ambao wameapa kuupinga mswada huo vikali bungeni, kulingana na tovuti ya IOL.

Upinzani unadai kuwa Zuma ni mfisadi na kuwa alimfuta kazi Pravin Gordhan kama waziri wa fedha, licha ya kuwa Gordhan aliheshimika sana.

Wanasema nia ya Zuma ilikuwa kuchukua usukani katika wizara ya fedha.

Zuma anakanusha madai ya ufisadi akisema kuwa yeye kufanya mabadiliko katika baraza la mawaziri na ni kwa manufaa ya raia

Kulingana na tovuti hiyo, Mbeki alisema kuwa wabunge wanafaa kuwa sauti ya wananchi na wala sio sauti ya vyama vya kisiasa.

Anasema huu ni wakati wa Afrika Kusini kujua ukweli kuhusu uhusiano wa kikatiba kati ya wananchi na viongozi wao wa kisiasa.

Mbeki ni mwanachama wa ANC ambaye alijiuzulu kama rais baada ya kupoteza imani kwa chama hicho kinachoongozwa na Zuma, mwaka wa 2008.

Chanzo: BBC
 
Zuma ni kama viongozi wengi wa Africa ameshaona nguvu yake ndani ya chama inapungua hasa ushawishi wake na pia ktk kuandaa Mazingira ya mrithi wake ambae anataka hasipate upinzani na mtu ambae inaonyesha anaweza kuwa mpinzani na mwenye ushawishi mkubwa ndani ya chama ni Pravin Gordhan

Tukumbuke mwezi wa December kuna mkutano mkuu wa ANC pia kumekuwa na vuguvugu la kumpigia kura ya kuto kuwa na imani nae ndani ya bunge sasa hatari ni kuwa kama watakubali kupiga kura ya siri si ya wazi, Zuma nafasi yake ya kuendelea kama rais wa SA ni ndogo sana
 
Back
Top Bottom