TFF yamburuta Hajji Manara kwenye Kamati ya Maadili

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Kwa mujibu wa Katiba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kila mwanafamilia wa mpira wa miguu Tanzania analazimika kuheshimu na kufuata kanuni za maadili za shirikisho kama zilivyoainishwa kwenye kanuni zake mbali mbali.

Wanafamilia wa mpira wa miguu ni pamoja na wachezaji, makocha, waamuzi, viongozi wa mpira wa ngazi zote na waajiriwa wa taasisi ambazo ni wanachama wa TFF wa ngazi mbalimbali.

Ili kutunza heshima ya mpira wa miguu Tanzania, wanafamilia wa mchezo huo katika kutimiza masharti ya kanuni za maadili za TFF, hawana budi kuheshimu na kufuata taratibu zote hizo ndani na nje ya uwanja.

Taswira njema ya shirikisho inajenga imani ya wadau wakiwamo serikali, mashirika mbalimbali ya umma na binafsi, vyombo vya habari, vyama vya mpira vya kimataifa, NGO’s na watu binafsi kwa taasisi (TFF). Kinyume chake ni kulibomoa shirikisho.

Dhima ya uongozi wa TFF ni pamoja na kulinda na kutunza heshima hii. Hivyo vitendo vyovyote vyenye viashiria vya uvunjaji wa maadili havitavumiliwa, na vikitokea hatua zitachukulia.

Na kwa muktadha huu Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania, limemfungulia mashtaka ya kinidhamu Msemaji wa Simba Bw. Hajji Manara kwenye Kamati ya Maadili. Leo hii Aprili 21, 2017 atapewa mashtaka yake na kujulishwa lini na wapi yatasikilizwa.

TFF inaendelea kutoa rai kwa wadau wa mpira kuwa pamoja ni kwamba ni haki yao kushauri, kupendekeza, kukosoa lakini yote haya yafanyike kwa staha ili kutunza heshima ya mpira wetu.
 
Kwa mujibu wa Katiba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kila mwanafamilia wa mpira wa miguu Tanzania analazimika kuheshimu na kufuata kanuni za maadili za shirikisho kama zilivyoainishwa kwenye kanuni zake mbali mbali.

Wanafamilia wa mpira wa miguu ni pamoja na wachezaji, makocha, waamuzi, viongozi wa mpira wa ngazi zote na waajiriwa wa taasisi ambazo ni wanachama wa TFF wa ngazi mbalimbali.

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
TFF YAMPELEKA HAJI MANARA KAMATI YA NIDHAMU
 
Haya akabutue hilo bakuli la mboga mbele ya kamati ya maadili.
TFF ni Yanga hamna jipya Malinzi? mwesigwa? Wambura? Lukas? Bure kabisa wala aibu hakuna
Kwa mujibu wa Katiba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kila mwanafamilia wa mpira wa miguu Tanzania analazimika kuheshimu na kufuata kanuni za maadili za shirikisho kama zilivyoainishwa kwenye kanuni zake mbali mbali.

Wanafamilia wa mpira wa miguu ni pamoja na wachezaji, makocha, waamuzi, viongozi wa mpira wa ngazi zote na waajiriwa wa taasisi ambazo ni wanachama wa TFF wa ngazi mbalimbali.

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
TFF YAMPELEKA HAJI MANARA KAMATI YA NIDHAMU
 
Mleta mada umeweka font size kubwa, kwani umeambiwa tuna matatizo ya macho?:(:(:(
Au na wewe ndo walewale?????
 
TFF ni Yanga hamna jipya Malinzi? mwesigwa? Wambura? Lukas? Bure kabisa wala aibu hakuna
Ingekuwa hivyo Jerry Muro asingefungiwa. Mkuu OSOKONI tuweke kando unazi kwa heshima ya mchezo wa soka. Ningeshangaa kama maneno hayo yangepita hivi hivi.

Mikia fc tulieni haki itendeke! Manara amekuwa akiimba amem_miss sana Jerry Muro naona kaamua kumfuata ili wakachati huko huko!

Big up TFF (Jamal Malinzi), hakuna double standard katika hili, hukumu na iteremke kama maji, amina.
 
Eti ili kulinda heshima ya mpira wetu..........! Mpira upi? Heshima ya mpira inapatikana uwanjani au kwa maneno mengi kama huo waraka wenu wa kipuuzi, kila siku mmeshindwa kusimamia ligi na mpira, mmetanguliza mahaba na matumbo yenu, kila siku matatizo Kwny mpira, rushwa chungumzima, ratiba haieleweki, rekodi za Kadi tu hamna, eti mnaita shirikisho sijui la upuuzi gani?

Vitu kama hiyo Kadi ya njano si vingekuwa vinawekwa rekodi Kwny website tu ya hilo TFF, mnatumia fedha za wananchi kukaa vikao visivyo na tija.

Hii serikali nayo na vyombo vyake nashangaa sana, madudu kama haya na waziri yupo tu, takukuru wanakodoa mi macho tu, hovyo kabisa!
 
Back
Top Bottom