Tff yala hasara mechi ya brazil na taifa stars

Tff yala hasara mechi ya brazil na taifa stars

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,074
Reaction score
34,844

Chati ya mapato ya mechi hiyo


Shirikisho la Mpira nchini TFF leo limekubali kwamba limekula hasara kutokana na kuandaa mechi ya Brazil na Taifa Stars ambapo kiasi cha shilingi 1.6bn/- tu kati ya takriban 4bn/ zilizotarajiwa. Katibu Mkuu wa TFF Frederick Mwakalebela kasema sasa hivi jijini Dar kwamba Shirikisho hilo linajiandaa na mikakati ya kufunika hasara hiyo pamoja na kuweka mambo sawa.

Hakutaka kwenda kwa undani ni shilingi ngapi walikopa na toka wapi lakini kasema Brazil walilipwa pesa yao kwa muda uafaka na kwamba watoa huduma wote walishalipwa na hakuna mwenye kuidai TFF.
Kasema, hata hivyo, mechi hiyo na Brazil ilikuwa na faida kubwa ya muda mrefu, ikiwa ni pamoja ya wachezaji takriban 6 kufuatwa na mawakala wa timu za ulaya kuwataka. Pia amesema utalii utakuwa sana kwani wengi wanaulizia Tanzania.
 
Back
Top Bottom