TFF yaachana na Kim Poulsen

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,455
29,134
Siku moja baada ya Timu ya taifa ya Tanzania kufungwa goli 1-0 dhidi ya Uganda, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza kumuondoa Kocha wa Tanzania, Kim Poulsen kwenye benchi la Ufundi pamoja na Wasaidizi wake.

TFF imesema hatua hiyo imefikiswa baada ya makubaliano baina ya pande zote katika kikao cha pamoja, lakini Poulsen ataendelea kubaki katika timu za taifa za vijana hadi mkataba wake utakapomalizika.

Kwa sasa timu ya taifa ya wakubwa itakuwa chini ya uangalizi wa Kocha Hanour Janza akisaidiwa na Meck Maxime na Kocha wa makipa Juma Kaseja.

FB_IMG_16617765238662160.jpg
 
Baada ya kula 10% yao kiasi cha kutosha sasa wameamua kumtoa kafara, tatizo la nchi yetu ni kuingiza siasa kila sehemu,na kama mambo hayatobadilika tutashindwa kila mahali na kuishia kutafuta mtu wa kumuangushia jumba bovu kwa sababu watu wengi hivi sasa wanafuta nafasi za uongozi kwenye maeneo mengine kama kwenye michezo lengo lao likiwa kujitanga ili baadaye wagombee uongozi wa kisiasa.
 
Kufungwa kwa Starz kuna sababu nyingi..

- Morali ya timu naona imeshuka sana, siku hizi starz haina mvuto kabisa ikicheza hata hamu ya kutazama sina.

- Viwango vya wachezaji wetu, nao wengi wameshuka viwango, hawana ubora unaotakiwa kwenda nao kwenye timu ya taifa, huwa hawajitumi wameridhika sana.

Hapa sitaki kutupa lawama kwa TFF kwa kuruhusu wachezaji wengi toka nje, kwani hao wageni nao hufanya mazoezi yao pamoja na wazawa, mwisho wa siku kocha humpanga aliye bora, kocha hawezi kumpanga mzawa hata kama hana kiwango cha kuridhisha.

Uamuzi wa kumuondoa Kim naona ni sahihi, wacha apumzike mzee wa watu, mazingira aliyokutana nayo wakati huu sio sawa na yale ya wakati ule alipofanikiwa kutengeneza vijana wenye vipaji, leo mambo yamevurugika, wachezaji wengi wa sasa hawaeleweki, hata wanaocheza nje.

  • Samatta kiwango kimeshuka.
  • Msuva haeleweki.
  • Ulimwengu haeleweki.
 
Wachezaji wetu viwango bado. Input ndio huzalisha Output, Sasa sisi tunataka tukiweka Mahindi kwenye mashine ya kukoboa itokee mchele, haiwezekani hii.

Mwishowe usipopata Mchele unasema mashine mbovu ibadilishwe, ujuha huu. Tuwekeze kwenye soka la vijana, wachezaji wetu ni kama mpira wamejulia ukubwani.
 
Siku moja baada ya Timu ya taifa ya Tanzania kufungwa goli 1-0 dhidi ya Uganda, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza kumuondoa Kocha wa Tanzania, Kim Poulsen kwenye benchi la Ufundi pamoja na Wasaidizi wake.

TFF imesema hatua hiyo imefikiswa baada ya makubaliano baina ya pande zote katika kikao cha pamoja, lakini Poulsen ataendelea kubaki katika timu za taifa za vijana hadi mkataba wake utakapomalizika.

Kwa sasa timu ya taifa ya wakubwa itakuwa chini ya uangalizi wa Kocha Hanour Janza akisaidiwa na Meck Maxime na Kocha wa makipa Juma Kaseja.

Aende akiendaga
 
Nikadhani Karia ndiyo angeanza kujiweka pembeni?
Na yule chawa wake Oscar Mirambo, walitakiwa kwa pamoja kujiondoa ili kuwaachia wenye mpira wao.

Miaka nenda wanapiga tu hela pale TFF! Hakuna mkakati wa kueleweka kwenye soka la vijana! Ona sasa, timu inacheza ikiwa haina kabisa morali! Yaani wachezaji wanacheza tu bora liende!! Hakuna muunganiko uwanjani! Hovyo kabisa.

Kumuondoa kocha bado haiwezi kubadilisha chochote iwapo TFF yenyewe imejaa wanasiasa, badala ya wanamichezo.
 
Back
Top Bottom