TFF - Weka maslahi ya taifa mbele!!!

Swala la adhabu alihusiani na upeo ni kuzingatia zaidi sheria, kanuni na taratibu. Kwa hiyo kukosea ndio kunakouhusiana zaidi na upeo, inawezekena upeo wa viongozi wa yanga ni mdogo ndio maana wakakosea kupeleka timu uwanjani. Kwa kuwa viongozi wa Yanga wamekosea haina maana na viongozi wa TFF nao wakosee kufuata sheria, kanuni na taratibu. Wanapokesea viongozi wa TFF nao pia watakuwa na upeo mdogo katika kushughulikia matatizo, uongozi sio tu neema siku zote.

Kukosea kwa Yanga pia sio kigezo cha kuwakandamiza katika kila adhabu kwa upeo mdogo wa watu. Wamekosea zifuatwe sheria, kanuni na taratibu za kuadhibu kuliko kuacha kila mtu ashauri anavyoona yeye inafaa. Wangapi wamekosea kabla na baada ya kristo na wakasamehewa au kuhukumiwa mpaka kukosea yanga ionekane aiwezekani?

Watoa hoja punguzeni jazba na unazi ili mtoe vifungu vitakavyo saidia kutatua mzozo huu.
 
Back
Top Bottom