TFF WANATAKA KUMHUJUMU SAMATTA,by Malisa GJ

Se-ronga

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
650
909
Hii nchi kuna watu wanapaswa kufungwa au
kupewa adhabu kali iwe fundisho. Miongoni
mwao ni Rais wa TFF Jamal Malinzi na safu yake
ya uongozi. Ningekua na mamlaka Malinzi leo
angelala "Keko au Segerea"..
Mbwana Sammata ameleta HESHIMA KUBWA
sana Tanzania ambayo viongozi wa kisiasa
wameshindwa kutuletea kwa miaka zaidi ya 50.
Ushindi wa tuzo ya Mwanasoka bora wa Afrika
kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani ni
ushindi mkubwa sana kwa taifa letu. Sammata
ameitangaza nchi yetu kwa kiwango kikubwa
sana. Waliokua hawaijui Tanzanua sasa wataijua
bila kupenda.
Brother Anthony Mtaka ambaye ni mwanasiasa
hodari, msomi na miongoni mwa watu
wachache ndani ya CCM wanaonivutia kisiasa;
amesema kuwa Sammata ametangaza Tanzania
vizuri kuliko viongozi wa Serikali waliotumia
mabilioni ya fedha kwa miaka kumi mfululizo
(2005 -2015) kutangaza vivutio vya utalii na
wakashindwa.
Ni wazi kuwa heshima aliyotupa Sammata ni
kubwa sana na tunapaswa kuheshimu mchango
wake hasa ukizingatia kwamba amefika hapo
kwa juhudi binafsi. Sio TFF wala Serikali
zilizochangia mafanikio ya Sammata. Ni yeye
mwenyewe na Mungu wake.
So ilitakiwa TFF waweke utaratibu mzuri wa
kumpokea Samatta kwa heshima. Ikiwezekana
watu wafanye maandamano ya amani kuanzia
pale Airport wanapompokea hadi mahali
watakapokutanikia. Kama tunaandamana kwa
sababu za kisiasa kwanini tusiandamane
kumpongeza mtanzania mwenzetu aliyeitangaza
vema nchi yetu kimataifa?
Tena ingepaswa tuwe na Media Campaign
maalum ya kumpongeza Samatta. Na tufanye
"hashtag" kwenye mitandao ya kijamii kama
FB, Tweeter, Instagram etc. Tujenge ushawishi
watu wajitokeze kwa wingi uwanja wa ndege wa
JNIA hadi Sammata mwenyewe asikie fahari na
ajivunie kuwa Mtanzania.
Lakini cha ajabu TFF kwa kushirikiana na CAF
wameamua kumhujumu Samatta. Na serikali
imekaa kimya as if ni sawa. Rais wa TFF Jamal
Malinzi ameandika kupitia ukurasa wake wa
Tweeter kuwa Samatta atatua nchini saa 8 za
usiku kesho jumamosi. Seriously?? Saa 8
usiku?? Apokelewe na "wanga" au??
Rafiki yangu Ezekiel Kamwaga amehoji kwanini
isitafutwe ndege ya saa 4 asubuhi kesho ili
watu waweze kujitokeza kwa wingi kumpokea?
Hivi kweli hatuwezi kum-market shujaa wetu??
Kama tulishindwa kumsaidia kufika hapo
alipofika, hata kumfanyia marketing
tunashindwa? Hivi mnadhani Samatta angekua
Mkenya angepokelewa saa 8 za usiku?? TFF
kuweni serious kidogo, acheni ujinga.!
Saa 8 za usiku watu wanakoroma vitandani,
wengine wako club wameshalewa "ndovu
baridi" ndio mmeona ni muda mzuri wa
kumpokea Sammata? Wanaopokelewa usiku wa
manane ni "majambazi" sio shujaa kama
Samatta.
Halafu Malinzi kwa kujishtukia anajaribu
kupunguza ukali wa maneno na kusema eti
Sammata atatua kesho "saa 8 alfajiri". Hakuna
kitu kinachoitwa "saa 8 alfajiri" kwenye
Kiswahili. Ni saa 8 usiku. Alfajiri inaanza saa
10. Sasa hiyo alfajiri ya Malinzi ya saa 8 usiku
ameitoa wapi?
Pia utetezi wa Malinzi ni wa "kitoto sana". Sio
utetezi wa kiongozi tena wa taasisi kubwa kama
TFF. Malinzi anasema saa 8 usiku ndio muda
ambao Sammata amekatiwa ticket na Shirikisho
ls Soka Afrika (CAF ) ambaao ndio waandaaji wa
tuzo hizo. Hivi kwani kila wanachofanya CAF
lazima tukubaliane nacho bila kuhoji?
Ilipaswa TFF wajiulize kwanini CAF wamemkatia
Samnata ndege ya usiku wakati ndege za
asubuhi au mchana zipo.?? Jibu ni rahisi tu
kwamba CAF wanaendeleza juhudi zao za
kuhujumu nchi za Afrika Mashariki. Hawapendi
kabisa kuona nchi zetu za Afrika Mashariki
zikifanikiwa kisoka. Ndio maana hata kwenye
michuano ya kimataifa wamekua wakitupanga
na timu ngumu kama "Ghana, Senegal,
Cameroon, Algeria, Misri, Nigeria" etc ili
tusifike mbali.
Kwahiyo hili la kumpangia Sammata kurudi saa
8 usiku sio bahati mbaya. Itz a planned and
organized matter. Lengo lao tushindwe kumpa
Sammata mapokezi mazuri na ya heshima.
Kwahiyo ilitakiwa viongozi wa TFF waione
hujuma hii na waikatae.
Sifa ya kiongozi (Leader) ni kuona pale ambapo
wengine hawawezi kuona. So TFF walitakiwa
waone kuwa muda aliopangiwa Sammata (saa 8
usiku) ni hujuma za CAF, then wafikirie mbinu
mbadala ya kukataa hujuma hiyo. Ikiwezekana
kumfanyia booking upya Samatta ili atue nchini
Asubuhi, Mchana au jioni muda ambao watu
wengi wanaweza kujitokeza kumpokea.
Lakini viongozi wa TFF wanakaa na vitambi
vyao vya "majani ya chai" wanakubaliana tu na
CAF bila hata kufikiri kidogo. Huu ni ujinga
ambao hata Mwenyekiti wa "vichaa duniani"
hawezi kuufanya.
Ingekua Sammata ni mKenya; kwanza
wangekataa hiyo ticket ya CAF ya saa 8 usiku.
Then wangemfanyia booking upya Samatta kwa
pesa zao ili aweze kutua kwa muda wanaotaka
wao. Na ingewezekana wangemtumia hata
ndege maalumu ya kwenda kumchukua.
Lakini hapa bongo TFF wamekaa tu kama
"mazuzu" wanakimbilia kuandika Tweeter bila
aibu eti Samatta atatua kesho saa 8 usiku. Nani
akampokee saa 8 usiku?? Labda Malinzi na
familia yake.
MY TAKE.!
Natoa wito kwa watumiaji wote wa mitandao
Tushikamane kwa umoja wetu bila kujali vyama
vyetu, dini, kabila au timu tunazoshabikia,
tupige kelele mitandaoni kuhakikisha Samatta
anatua nchini muda ambao watanzania
tunaweza kwenda kumpokea.
Kama itakosekana ndege ya kesho mchana bora
aje Jumapili asubuhi kuliko kuja hiyo kesho saa
8 usiku. Share ujumbe huu, mtag kiongozi
yeyote wa Serikali au wa TFF. Kama una namba
zao wapigie au watumie sms kuonesha kulaani
hujuma inayotaka kufanywa dhidi ya Sammata
ya kumpokea saa 8 za usiku.
Tunamtaka Sammata muda ambao tunaweza
kumpokea sio saa 8 za usiku.
# JUSTICE_4_SAMMATA .!
 
Hizi habari kama ni za kweli,hakika zitatukera wengi!
 
Hamna haja ya kupanic, hizi ni logistics ndogo tu. Rearrangement ifanyike basi.
 
Tz ndo ilivyogo kila kitu nginjinginji! Wema wafa mapema wabaya mbona hamdanji?? Ukabila! Rushwa! maofisini ndo swadakta! Alikua dokta wa mifugo leo hii katibu wa soka!!! Naimba tu.
 
Tuna ndege ya rais GULF STREAM ONE ina uwezo wa kwenda nigeria kwa masaa manne na nusu hadi matano.kwa heshima aliyoiletea Tanzania MBWANA SAMATTA alipaswa kupewa heshima inayostahili tena media zote kama bbc,aljazeera,cnn,voa,rt,france24 etc zialikwe wakati wa mapokezi.hii ingekuwa moja ya fursa ya kuitangaza nchi.kwani kuna baadhi ya mitandao ya kijamii ya nje imemuandika samatta kama raia wa botswana na nyingine kama tunisia
SAMATTA ANAPASWA KUPEWA HESHIMA KUBWA SANA NA NCHI HII
IMG-20160108-WA0006.jpg
IMG-20160108-WA0005.jpg
IMG-20160108-WA0006.jpg
IMG-20160108-WA0005.jpg
 
Dah! mkuu umetiririka ukweli mtupu,kuna wale wanaokwendaga olimpik wanarudi mikono mitupu but hawarudi muda ambao shujaa kama samatta anavyorudi, soka la bongo ni ubabaishaji mtupu,hakuna ambaye anaweza kututoa huku tulipo kama hatutachagua viongozi ambao michezo iko damuni lakini sio hawa waliopo.
 
Akafatwe na GULF STREAM,tuko radhi tule nyasi.Kama hakuna mafuta watoe namba ya m-pesa tudundulize.Heshima aliyeleta Samatta kwa nchi yake haina kifani.Bravo Samatta
 
Back
Top Bottom