TFF, Uganda sio mbali...

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,321
4,671
Nianze kwa kutoa Pongezi kwa Shirikisho la Mpira Uganda(FUFA),Jopo zima la Ufundi Timu ya Taifa chini ya Mtaalamu Micho Kashafundisha Yanga Huyu Na Kwa Timu Ya Taifa Ya Uganda(Uganda Cranes) kwa kufanikiwa Kushiriki Kombe la Mataifa Huru Afrika Na pia Kuibuka Timu Bora Ya Mwaka Kwa upande wa Tuzo za Caf.

Kwa Mafanikio yote hayo shirikisho letu la Mpira (TFF) Wanakitu kikubwa sana cha kujifunza Toka Uganda Mafanikio Ya Uganda hayajaja kama Uyoga bali ni kupitia Uwekezaji Makini Kwenye Soka Na Mipango Endelevu,Hawa Uganda tulikua Kundi moja lakini wenzetu leo wamepiga hatua kubwa kwenda Mbali Wakati Sisi tunapiga hatua Kurudi Nyuma.

Hawa Uganda kama kumbukumbu ziko vizuri tulicheza nao katika hatua za kutafuta timu itakayoshiriki michuano ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani(CHAN) Pale kwao Nakivubo Athumani Iddi Chuji Akafunga goli zuri sana na Kufanikiwa kuwatoa Uganda ila Leo Sidhani hata tuna Ubavu huo tena hapa kwetu wenyewe wanatufunga.

Na kama Sikosei Leo au kesho Uganda Cranes wanacheza Na Slovakia mechi ya kujipima Nguvu

Ushauri kwa TFF hakuna Haja ya kutuma Watu Brazil kujifunza wao wanatumia mbinu gani tuanze kwa hawa Majirani zetu Watusaidie Wao wametumia Mbinu gani mpaka kufanikiwa.
 
Bongo ni sikio la kufa, wewe rais mshauri wake wa maswala ya ufundi hajawahi kucheza mpira daraja lolote, hajawahi kufundisha wala hata kuhudhuria kozi yoyote ya mpira, kamuweka pale kwa sababu kukaya, alafu unategemea, rais malinzi atakuwa na vision gani ya kuufanya mpira uendelee, ikiwa yy mwenyewe kakubali kushauriwa na kipofu. TFF imejaa wahuni kibao wasio ujua mpira huku watu wanaoufaham mpira wamewekwa pembeni. Ukija ktk vilabu vyetu hivi vikubwa nao hovyo, ukimaliza na mlezi wao BMT,nae haeleweki watu wanataka kuwekeza wanaleta upuuzi wao, sijui kwa sababu wanajua watakosa mgao. BMT wako bize kutatua migogoro ya simba na yanga lkn migogoro ya chaguzi zinazofanyika ktk chaguzi hizi za mikoani na wilayani wamekaa kimya, yaani system ya mpira ipo hovyo, mimi natamani serikali nguvu yake ihamishie ktk michezo mingine, mpira wa miguu waachane nao.
 
Back
Top Bottom