TFF ligi ijayo Sio lazima kila mchezo uanze saa kumi.

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,321
4,671
Asilimia kubwa ya michezo ya ligi inachezwa saa Kumi adhuhuri isipokuwa kidogo ile ya timu ya Azam inayochezwa saa moja jioni.

Sioni Sababu ya michezo yote kuchezwa muda mmoja wa saa kumi ni Vyema ligi iyajo Tff mjitaidi kupanga ratiba tofauti angalau baadhi ya michezo ichezwe hata jioni sio Vibaya hata siku moja labda mchezo wa Simba Vs Yanga ukachezwa hata mida ya saa 12 jioni au hata saa moja jioni na hata michezo mingine.

Kwa muda mrefu jirani zetu Zanzibar baadhi ya michezo imekua ikichezwa usiku hata lile kombe la muungano michezo mingi huchezwa usiku na mashabiki hufurika Uwanjani,ni kujipanga tuu Sidhani kama litashindikana hili Tff mkiamua.
 
Shida ya kuwa na viongozi ambao si wabunifu, business as usual
 
Wanaogopa gharama za kulipia umeme.
unakuta weekend michezo yote inachezwa muda mmoja na kwisha muda mmoja unakosa hata kitu cha kuangalia,Nafikiri wakihamasisha watu kupenda mpira na kuingia viwanjani sidhani kama watashindwa kulipa bili za umeme
 
1494489364238.png

Hii imekaa vizuri naona mmeanza kutenda kwa vitendo game itaanza saa 12:00 jioni badala ya 10:00 je Mbeya City atakubali kuwa ngazi ya Yanga kuelekea kwenye Ubingwa?tusubiri.
 
Na TFF ihakikishe wana pata mdhamini mzuri amabaye atahakikisha timu zote zina safiri kwa usafiri wa anga ili kuwahi michezo yao. ATCL igo gado kuhakikisha usafiri wa haraka.
 
Kwa uongozi huu wa Malinzi hapawezi kuwa na maendeleo makubwa ya ubunifu kama vitu vidogo tu vya usimamizi wa sheria na kanuni vinashindwa kufanyika. Vipaumbele vyao ni kufungia watu, kujitetea dhidi ya tuhuma za ukabila, na upigaji

Ligi ingeongezeka sana msisimko kama vitu hivi vingefanyika, na ni kwa uchache;

1. Uwanja wa Azam Complex kutumika kwa mechi za Simba na Yanga
2. Mechi kupishanishwa muda, hasa za Uwanja wa Taifa kuchezwa jioni kuelekea usiku
3. Mechi kubwa kupishanishwa muda na zile za Ulaya
4. Simba na Yanga kuchezwa pekee kwa siku hiyo
5. Ratiba kutoruhusu timu moja kucheza mechi zaidi ya 2 mfululizo kwenye uwanja wake wa nyumbani
6. Mechi zote kurushwa live bila kisingizio chochote
 
Website ya TFF nimejaribu kuifungua , browser yangu inaniambia kuwa website ya tff imepandwa malware hatari...kule cafonline.com huko naona wamepigwa DDOS week ya tatu sasa hawako hewani! Sijui nao Issa Hayatou kakasirika kaamua kuondoka nayo sijui nini. TFF mnatakiwa mtupe update juu ya kinachoedelea kwenye kambi ya timu yetu ya U17 huko Gaboni!
 
Kwa uongozi huu wa Malinzi hapawezi kuwa na maendeleo makubwa ya ubunifu kama vitu vidogo tu vya usimamizi wa sheria na kanuni vinashindwa kufanyika. Vipaumbele vyao ni kufungia watu, kujitetea dhidi ya tuhuma za ukabila, na upigaji

Ligi ingeongezeka sana msisimko kama vitu hivi vingefanyika, na ni kwa uchache;

1. Uwanja wa Azam Complex kutumika kwa mechi za Simba na Yanga
2. Mechi kupishanishwa muda, hasa za Uwanja wa Taifa kuchezwa jioni kuelekea usiku
3. Mechi kubwa kupishanishwa muda na zile za Ulaya
4. Simba na Yanga kuchezwa pekee kwa siku hiyo
5. Ratiba kutoruhusu timu moja kucheza mechi zaidi ya 2 mfululizo kwenye uwanja wake wa nyumbani
6. Mechi zote kurushwa live bila kisingizio chochote
Ushauri Kuntu,unakuta Simba na Yanga wanacheza Siku moja na mechi ya Mbeya city vs Prison Pale Taifa uwanja unajaa kule Sokoine watu kumi hapa lazima Vilabu vitalia na Ukata tuu wawe wakiweka mida tofauti kwa zile mechi kubwa.
 
Hali ya hewa na miundombinu ndo sababu

Maeneo mengi kuna jua Kali kabla ya saa kumi. Lazima wasubir kwanza lipoe

Pia umeme ni tatizo viwanja vingapi vinaweza kuwasha taa watu wakacheza ?? Bila shaka ni taifa, kwa bb huenda chamanzi au kilumba tu. Navyo umeme wake si wa uhakika

Suala la mashabiki nalo ...watanzania walio wengi wanafanya kazi mpaka saa Tisa na ndio haohao wanaoangalia Mpira. Ukiwanyima fursa kwa kuweka mechi Mapema unaikosesha klabu mapata yanayoisaidia kuendeshwa.
 
Na TFF ihakikishe wana pata mdhamini mzuri amabaye atahakikisha timu zote zina safiri kwa usafiri wa anga ili kuwahi michezo yao. ATCL igo gado kuhakikisha usafiri wa haraka.
Hili baadaye sana....Mpira bado upo chini haiwezekani kupata wadhamini ghali kiasi hicho wakati faida ni kiduchu.
 
Hali ya hewa na miundombinu ndo sababu

Maeneo mengi kuna jua Kali kabla ya saa kumi. Lazima wasubir kwanza lipoe

Pia umeme ni tatizo viwanja vingapi vinaweza kuwasha taa watu wakacheza ?? Bila shaka ni taifa, kwa bb huenda chamanzi au kilumba tu. Navyo umeme wake si wa uhakika

Suala la mashabiki nalo ...watanzania walio wengi wanafanya kazi mpaka saa Tisa na ndio haohao wanaoangalia Mpira. Ukiwanyima fursa kwa kuweka mechi Mapema unaikosesha klabu mapata yanayoisaidia kuendeshwa.
nimeshauri iwe Jion zaidi badala ya mechi zote kuchezwa saa kumi na pia suala la kuanza mapema mbona michuano ya kagame cup au cecafa baadhi ya mechi huanza saa nane na zinachezwa vizuri tu

Inabd hizi timu zijifunze mazingira tofauti utakataa kucheza hapa saa nane utaenda Sudan mchezo unachezwa saa Saba wakifungwa sababu kuu tumecheza mchana.

Kuhusu Viwanja ni suala la Tff na Serikali au chama mmiliki wa viwanja kufanya ukarabati wa viwanja kuhakikisha miundombinu yote muhimu inapatika ikiwemo umeme wa uhakika

Tff kuna fungu wanapata toka Fifa pia kuna udhamini mkubwa sana kipindi hiki kwanini wasiwekeze kwenye ukarabati wa Viwanja?
 
Tusiwalaumu TFF, je umeme wetu ni wa uwakika? Umeme Tanzania ni shida una katika katika muda wowote na bila taarifa. He tunamajenereta ya kutosha viwanja vyetu pindi umeme ukikata?
 
Kinachosababisha umeme usiwe wa uhakika ni nini haswaa,Tukitaka tupige hatua kwenye soka letu lazima tukubali kugaramia
 
nimeshauri iwe Jion zaidi badala ya mechi zote kuchezwa saa kumi na pia suala la kuanza mapema mbona michuano ya kagame cup au cecafa baadhi ya mechi huanza saa nane na zinachezwa vizuri tu

Inabd hizi timu zijifunze mazingira tofauti utakataa kucheza hapa saa nane utaenda Sudan mchezo unachezwa saa Saba wakifungwa sababu kuu tumecheza mchana.

Kuhusu Viwanja ni suala la Tff na Serikali au chama mmiliki wa viwanja kufanya ukarabati wa viwanja kuhakikisha miundombinu yote muhimu inapatika ikiwemo umeme wa uhakika

Tff kuna fungu wanapata toka Fifa pia kuna udhamini mkubwa sana kipindi hiki kwanini wasiwekeze kwenye ukarabati wa Viwanja?
Kagema inachezwa sababu ya mda kuwa mfupi na hasara yake mapato n kdogo

Kumbuka Mpira ni kazi watu wanataka faida. Unapoweka mda ambao watazamaji wapo busy inakula kwako. Ndo maana hata uingereza katikati ya wiki mechi zote ni baada ya kazi saa 1 kwa mda wa kwao ambapo watu wameshatoka kazini
 
Back
Top Bottom