TFF kutumia muda mwingi kwenye PRESS . . . . . | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TFF kutumia muda mwingi kwenye PRESS . . . . .

Discussion in 'Sports' started by CPU, Oct 4, 2011.

 1. CPU

  CPU JF Gold Member

  #1
  Oct 4, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  WIKI mbili zilizopita, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Chilla Tenga alikutana na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini kujaribu kuwekana sawa katika masuala mbalimbali yanayouzunguka mchezo wa soka nchini.

  Pamoja na ufafanuzi mwingi uliotolewa na Rais Tenga pamoja na katibu wake, Angetile Osiah bado kuna umuhimu wa kujikumbusha jinsi ambavyo katika siku za karibuni, TFF imekuwa ikitumia muda mwingi wa kutoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo kuliko kutoa taarifa za maendeleo.

  Kutoa ufafanuzi wa adhabu za akina Louis Sendeu, Ismail Aden Rage, nembo ya klabu ya African Lyon, logo nyeusi ya Vodacom katika jezi za Yanga na mengineyo zisionekane kama ndio kazi za kila siku za TFF katika soka letu. Tunahitaji kusikia habari chanya zaidi katika soka letu.

  Tunahitaji kusikia TFF ikitoa habari kuhusu upatikanaji wa mikataba ya kisasa katika soka la vijana. Tunahitaji kusikia TFF ikitoa taarifa kuwa imepata nafasi za kupeleka makocha wetu nje kwa ajili ya kupata utaalamu. Tunahitaji kusikia TFF imepata udhamini wa jezi kutoka kampuni kama Nike, Puma, Adidas na mengineyo
   
Loading...