Akiteketeza kwa moto kilo themanini na nne za nyama ya Ng'ombe ambayo ilikutwa ikiuzwa katika mazingira machafu huku ikiwa imehifadhiwa chini,mkaguzi wa chakula kutoka TFDA kanda ya kati Bwana Aberl Deule, amesema wamefikia uamuzi wa kuteketeza nyama hiyo kwa sababu licha ya machinjio kufungwa baadhi ya wafanya biashara wanachinja ng'ombe vichochoroni na kuhatarisha maisha ya walaji.
Wachinjaji wanyama wa manispaa ya Singida wametupia lawama kwa mkurugenzi wa manispaa ya Singida kuacha kufanyia matengenezo na usababisha machinjio kufungwa mara kwa mara ,huku wao wakiwa wamekopa fedha katika sekta za benki.
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Singida Bwana Deusi Luziga amekiri kuwa machinjio hayapo katika hali nzuri,ila manispaa imeanza kufanya ukarabati wa machinjio hayo na wameshatenga eneo la kujenga chinjio jingine jipya kulingana na kuongeeka kwa watu.
Chanzo: ITV