Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,618
- 9,611
MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA), Ofisi ya Kanda ya Ziwa, imekifungia kwa muda kiwanda cha kutengeneza maji ya kunywa cha Kabanga Springs kilichoko Kamachumu, Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera.
Uamuzi wa kukifungia kiwanda hicho, umechukuliwa baada ya wakaguzi wa chakula wa TFDA Kanda ya Ziwa kubaini uapungufu makubwa ya usafi na utaalamu kinyume na kanuni za uandaaji wa chakula salama za mwaka 2006.
Akizungumza jana, Mkaguzi wa Chakula wa TFDA Kanda ya Ziwa, Nuru Mwasulama aliyataja upungufu huo kuwa ni uwapo wa vumbi katika mashine za kusindika, sakafuni na kwenye kuta za kiwanda hicho, wafanyakazi kutopimwa afya na kukosa sare, kukosekana kwa mfumo wa maji safi katika vyoo hali ambayo ilikuwa inasababisha uchafu katika eneo hilo.
Mwingine, ni uchakavu wa machujio ya maji katika sehemu ya kuchujia maji na kutofanya kazi kwa mfumo wa UV-Light hali ambayo inahatarisha usalama wa maji yanayozalishwa, uchafu uliokithiri katika maabara ya uchunguzi wa maji na kukosekana kwa taarifa zinazoonesha ufuatiliaji na upimaji wa ubora na usalama wa maji.
“Kutokana na mapungufu makubwa yaliyoonekana wakati wa ukaguzi na yanayokinzana kwa kiasi kikubwa na kanuni za usindikaji salama wa chakula tumesitisha shughuli zozote za usindikaji wa maji katika kiwanda mpaka watakapo fanya marekebisho muhimu,” alisema Mwasulama.
Alisema mamlaka hiyo,itakuwa tayari kukifungua kiwanda hicho pale ambapo itajiridhisha kuwa maelekezo yote yalitolewa yamefanyiwa kazi.
Aliyataja baadhi ya maelekezo yaliyotolewa kwa wamiliki wa kiwanda kuwa pamoja na kuwapima afya wafanyakazi, kubadirisha machujio ya maji, kutengeneza mfumo wa UV- Light unaotumika kuangamiza vijidudu hatarishi ili kuhakikisha usalama wa maji yanayozalishwa, kufanya usafi katika chumba cha maabara na kutunza kumbukumbu za maabara, kutafuta mtaalamu wa chakula mara moja kwa ajili ya kusimamia uzalishaji salama wa maji na kuwapatia wafanyakazi sare za kazi.
“Tumemuagiza atutaarifu kwa maandishi pale atakapo maliza utekelezaji wa maagizo yote tuliyompatia. Tutakapo jiridhisha kuwa ametekeleza maagizo ya mamlaka tutamfungulia ili aendelee na uzalishaji,” alisema Mwasulama.
Mtanzania