TFDA&TBS warushiana mpira kuhusu sidiria zenye vidonge na sponji ya maji maji

zubedayo_mchuzi

JF-Expert Member
Sep 2, 2011
4,873
1,217
Mwandishi Aziza Masoud ameripoti hofu juu ya uwepo wa sidiria ambazo zinaonekana kwenye clip za video hasa watsup kuwa na sponji ambazo zimeleta hofu kubwa kwa ndugu zetu wanaozitumia,

Mbali na hapo mwandishi alijaribu kuwatafuta wahusika hasa TBS,TFDA na wizara ya afya kupata maelezo kuhusu hizi taarifa, jambo kubwa la kushangaza ni juu hizi taasisi mbili kubwa ambazo ndizo msingi wa tatizo hili.

Nazungumzia TFDA na TBS, mwandishi alimtafuta msemaji wa shirika la viwango, ROIDA ANDUSAMILE, alisema pamoja na ofisi yake kuhusika na mambo yahusuyo viwango ofisi yake haina mamlaka ya kuzungumzia mambo yahusuyo madawa na pamoja na kuhusika kukagua bidha hiyo.

Naomba nimkumbushe tu kuwa shirika la viwango ndilo linalohusika na ukaguzi wa mizigo inayoingia nchini hasa kwa upande wa nguo nikimanisha mitumba au nguo mpya,shirika LA VIWANGO LILIPIGA MARUFUKU uingizwaji wa nguo za ndani zikiwemo chupi,sidiria,baada ya kuonekana si salama kwa matumizi ya binadamu,mara ya mwisho iliendesha msako kariakoo nzima chini ya ulinzi wa jeshi la polisi na kuzikamata bidhaa hizo za sidiria,msako huo ulisimamiwa na afisa wa TBS mwenye jina la manyilija.

Mwandishi alimtafuta msemaji wa TFDA bi Gaudensia Simwanza,alisema hawezi kutoa ufafanuzi kwasababu suara hilo haliwahusu, ni kweli sidiria haiwahusu TFDA lakini kidonge kidonge kilichopatikana ndani ya sidiria kina wahusu nyie TFDA, swala sio kunywa kwani vipodozo kuna watu wanakunywa hapana,kwasababu ni kidonge TFDA mlitakiwa mchukue sampuli hizo za vidonge hivyo mkavipime,vingine vikipelekwa kwa mkemia mkuu wa serikali.

Kitendo cha mashirika haya kutoa majibu ya kurushia mpira ni kutokuwepo kwa umakini wa kazi zao hasa linapotokea swala linalogusa taaasisi zote mbili.

Tena mwandishi alisahau kumtafuta msemaji wa tume ya mionzi,kwasababu kama kuna sponji zenye majimaji ni lazima tume ya mionzi nao watuambie kama maji hayo hayaja vyonza mionzi yoyote.

Chanzo: Mtanzania

.....Kwa hili taasisi zote tatu mje na majibu.

BY ZUBEDAYO_MCHUZI MZEE WA KUTEMBEA UMBALI MREFU.
 
Well said japo hapo kwenye sponji yenye majimaji bado tfda na tbs ndio wahusika wakuu. Hao watu wa mionzi na mkemia mkuu wanatakiwa tu kupelekewa samples ili kuona kuna nini ndani yake.
Na watueleze hvyo vitu kazi yake ni nn kwenye sidiria
 
Well said japo hapo kwenye sponji yenye majimaji bado tfda na tbs ndio wahusika wakuu. Hao watu wa mionzi na mkemia mkuu wanatakiwa tu kupelekewa samples ili kuona kuna nini ndani yake.
Na watueleze hvyo vitu kazi yake ni nn kwenye sidiria
Mkuu watu wa mionzi muhimu sana kwa sasa wapo bandarini kukagua mizigo yote yenye uwezo wa kufyonza mionzi,wanachukua sampuli na kwenda kupima.

kama hizo sponji zenye maji maji ni muhimu na mionzi wakatoa majibu,wasiwasi mkubwa ni kansa
 
Gazeti la mtanzania ukurasa wa pili 13/march/2016

Mwandishi AZIZA MASOUD ameripoti hofu juu ya uwepo wa sidiria ambazo zinaonekana kwenye clip za video hasa watsup kuwa na sponji ambazo zimeleta hofu kubwa kwa ndugu zetu wanaozitumia,

mbali na hapo mwandishi alijaribu kuwatafuta wahusika hasa tbs,tfda na wizara ya afya kupata maelezo kuhusu hizi taarifa,jambo kubwa la kushangaza ni juu hizi taasisi mbili kubwa ambazo ndizo msingi wa tatizo hili,nazungumzia tfda na tbs,mwandishi alimtafuta msemaji wa shirika la viwango, ROIDA ANDUSAMILE,Alisema pamoja na ofisi yake kuhusika na mambo yahusuyo viwango ofisi yake haina mamlaka ya kuzungumzia mambo yahusuyo madawa na pamoja na kuhusika kukagua bidha hiyo

Naomba nimkumbushe tu kuwa shirika la viwango ndilo linalohusika na ukaguzi wa mizigo inayoingia nchini hasa kwa upande wa nguo nikimanisha mitumba au nguo mpya,shirika LA VIWANGO LILIPIGA MARUFUKU uingizwaji wa nguo za ndani zikiwemo chupi,sidiria,baada ya kuonekana si salama kwa matumizi ya binadamu,mara ya mwisho iliendesha msako kariakoo nzima chini ya ulinzi wa jeshi la polisi na kuzikamata bidhaa hizo za sidiria,msako huo ulisimamiwa na afisa wa tbs mwenye jina la manyilija.

mwandishi alimtafuta msemaji wa tfda bi Gaudensia simwanza,alisema hawezi kutos ufafanuzi kwa sababu suara hilo haliwahusu,ni kweli sidiria haiwahusu tfda LAKINI kidonge kidonge kilichopatikana ndani ya sidiria kina wahusu nyie tfda,swala sio kunywa kwani vipodozo kuna watu wanakunywa hapana,kwa sababu ni kidonge tfda mlitakiwa mchukue sampuli hizo za vidonge hivyo mkavipime,vingine vikipelekwa kwa mkemia mkuu wa serikali.

kitendo cha mashirika haya kutoa majibu ya kurushia mpira ni kutokuwepo kwa umakini wa kazi zao hasa linapotokea swala linalogusa taaasisi zote mbili.

tena mwandishi alisahau kumtafuta msemaji wa tume ya mionzi,kwasababu kama kuna sponji zenye majimaji ni lazima tume ya mionzi nao watuambie kama maji hayo hayaja vyonza mionzi yoyote.

.....Kwa hili taasisi zote tatu mje na majibu.

BY ZUBEDAYO_MCHUZI MZEE WA KUTEMBEA UMBALI MREFU.
Tatizo kubwa la kuwa na utitiri wa Taasisi zenye majukumu na malengo yanayofanana. Kwenye raha mko wote, kwenye shida visingizio kibaooo! Ukimuuliza huyu atakwambia nenda kwa yule, ukienda kwa yule atakwambia rudi kuleee! Siku zinazidi kusonga na jamii inaathirika. Hapa kuna haja ya kuziangalia hizi Taasisi kama TFDA, TBS, Vipimo, Mkemia Mkuu wa Serikali, n.k kama zina malengo yanayofanana ziunganishwe. Ili pindi litokeapo tatizo kusiwe na mtindo wa kukwepa majukumu.
 
Back
Top Bottom