Ni kweli TFDA na TBS wanafanya kazi moja na siyo hao tu kuna taasisi zaidi ya saba zinafanya kazi moja. Kwa wenye viwanda ongeza OSHA, WMA, FIRE, NEMC, COUNCILS na nyinginezo. Ukizichunguza hizi taasisi zote zinarudia kile ambacho wengine wanafanya. Ukiwauliza wote wanasema wameanzishwa kwa sheria mbalimbali na wanatekeleza sheria. Hii imetokana na kucopy na kupaste sheria mbalimbali kutoka nchi tofauti kwa mfano tunacopy South Africa then tunaenda Ghana kumbe sheria ya South Africa imetake care hiyo sheria ya Ghana, Pia taasisi hizi hulipwa na wafanyabiashara kwahiyo serikalini hawaoni huo mzigo, ndiyo maana bidhaa za Tanzania zinakuwa ghali sana. Maoni yangu ni hizi taasisi zijiendeshe na fedha kutoka serikali kuu na siyo kwa fee au tuwe na taasisi moja au mbali kama mdau anavyoshauri hapo juu. Tanzania haiwezi kuwa nchi ya viwanda wakati kuna taasisi zaidi ya saba ambazo bila wao huwezi fungua kiwanda. NB TBS ndiyo sherika pekee lenye kutengeneza viwango na wote TFDA N.K Hutumia viwango vya TBS bidhaa inapimwa na TBS then TFDA parameter ni zile zile, standard ni hiyo hiyo, hii siyo tu gharama kwafanyabiashara bali pia matumizi mabaya ya wafanyakazi, vifaa na kemikali ambazo mara nyingi tunazinunua kwa fedha za kigeni.