TFDA: Hatuufahamu mchele wa plastiki

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,251
Sillo.jpg

Mkurugenzi wa TFDA, Hiiti Sillo

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na dawa {TFDA}, Hiiti Sillo amewatoa wasiwasi wananchi wa Tanzania kwa kuwaambia mpaka sasa hawajapokea taarifa yeyote ya kuonesha kuwa kuna mchele wa plastiki katika masoko makubwa na madogo ya mchele.

Siilo amebainisha hayo baada ya kuenea kwa uvumi katika mitandano ya kijamii ambao ulikuwa unasambaza taarifa za kuingizwa mchele feki wa plastiki katika masoko ya mchele pamoja na maduka ya reja reja

"TFDA imesajili mchele wa Basmati lakini siyo huo wa brand ya sunrice, ambao taarifa zake zimekuwa zikisambaa kwa madai ni mchele wa plastiki. hatuutambui na taarifa ile sisi tulipoipokea tulianza kufanya ukaguzi wa ufuatiliaji na kiuchunguzi, mchele tunaoufahamu ni ambao umelimwa mashambani umevunwa na ndiyo ambao tunautumia kwa hiyo hatujawahi kuona mchele unaotokana na plastiki kitaalamu hatujawahi kuufahamu" alisema Sillo.

Pamoja na hayo Sillo amewataka wananchi wawe majasiri katika kutoa taarifa za ukweli kuhusiana na tatizo hilo ili ziweze kuchukuliwa kwa haraka zisije kuathiri afya za watu.

"Tuwe wajasiri tusioneshe mikono pekee yake kwa sababu tutakuwa hatujawasaidia watu bado, unalalamika kuwa umekula chakula ambacho unahisi siyo bora lakini namna ambavyo ujumbe unatufikia haujatusaidia bado tunawaomba sana wananchi watupe taarifa, sisi tumejipanga na tutawafikia hao" alisisitiza Sillo.

Chanzo: Sillo
 
Tuwalinde watanzania, mchele wa chuma usiungwe mkono kwa vyovyote...

Wahusika washtakiwe vikali.
 
Duuuh kweli hatari zile video zilinitisha kweli nikinunua mchele lazima niukague sana
 
Nimeshindwa kusoma maelezo yote kutokana na kichwa cha habari kinavyo hasirisha!

Hivi kama wewe ni mtaalam, umepeewa kitengo cha kusimamia usalama wa walaji ndani ya Tanzania, tangu siku zote atu wanalalamika kuwa kuna mchele wa plastic, bila haya unakuja kusema huufahamu!. Kwa nini usiondoke kazini?

TFDA waondolewe ofisini kwa nguvu kama mteuzi wao hatawaondoa kwa sababu ni hatari kwa taifa!.

Nilitegemea scientific reasons za kwa nini huu hapa siyo mchele wa plastic kama watu wanavodhani.




TFDA waseme kwa utaalamu wao mchele huu wa plastic ni salama kwa chakula cha binadamu!.


KWA NINI TFDA WASHISTAKIWE?
 
Alafu mtu mmoja akiupiga marufuku tunandaa maandamano ya kupongeza!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom