Bigjahman
JF-Expert Member
- Jan 5, 2011
- 875
- 460
Mh.Rais, waheshimiwa Mawaziri wa afya pamoja na biashara, Mkurugenzi wa TAKUKURU Taifa, itifaki imezingatiwa.Sisi wafanyibiashara wa vipodozi mkoani Arusha tunasikitishwa sana na kero kubwa na unyanyasasaji tunaofanyiwa na TFDA Arusha.
Tunatambua majukumu makubwa taasisi hii ya Serikali imekabidhiwa ambayo ni kuhakikisha mwananchi anapata bidhaa salama za vyakula pamoja na dawa vikiwemo vipodozi. TFDA imekua ikiyatumia mamlaka haya vibaya kwa kutuonea na pia kutengeneza mazingira ya rushwa.
Tunaamini pia imehodhiwa na wafanyabiashara wasio waaminifu wanaotumia TFDA kurudisha wengine nyuma. Pia inakinzana na kauli mbiu ya mh. Rais ya kuwataka wafanyabiashara kuanzisha viwanda na pia kulipa kodi mfano mkubwa tulio nao ni jinsi TFDA Arusha wanavyoinyanyasa kampuni ya BYC pamoja na mmoja wa wamiliki wake ndg Philemon Kitundu ambae pia anamiliki duka la vipodozi la Philemon Cosmetics lililopo mitaa ya Bondeni mjini hapa.
Kwa kifupi Philemon pamoja na wenzie wawili walisajili kampuni ya BYC Company Ltd ambayo ilizamiria kutengeneza mafuta ya kujipaka binadamu. TFDA walifanya ukaguzi katika eneo ampapo wangefungua kiwanda na kulithibitisha na waliwaelekeza BYC wafanye malipo ili wawape kibali lakini cha kushangaza iliwachukua takribani mwaka mzima na TFDA hawakutoa kibali.
Eneo lile lile lilibaki tupu muda wote huo bila kazi yeyote na ndipo Philemon cos walilitumia kuhifadhi bidhaa zao za dukani. Katika hali ya taharuki TFDA walifika pale na kuzikamata kwa madai pale sio ghala la kuhifadhi bidhaa hizo. Bidhaa zilikua na thamani ya takribani milion 58. Waliwaelekeza waandike barua ili wapewe bidhaa hizo.
Philemon pamoja na BYC walifanya hivyo lakini hawakurudishiwa bidhaa zile baada ya kuhangaika bila mafanikio, bidhaa zile zilianza kuuzwa madukani na Philemon pamoja na BYC walipofatilia hawakupata jibu sahihi. Waliamua kwenda TAKUKURU Arusha. Tunaishukuru TAKUKURU kwani walifanya kazi yao kwa umakini na walifika TFDA na kukuta kweli catoni 86 hazipo, na zimepotea katika mazingira ya kutatanisha. TFDA walipoona haya yametokea walileta tuhuma mpya kwamba
(1) Mzigo ule umetoka nje nchi na hauna vibali vya kuingia hapa nchini. Tuhuma hizi si za kweli kwani mzigo ulinunuliwa katika viwanda vya Dar mfano Chemi Cotex pamoja na maduka makubwa yaliyopo Dar e Salaam na stakabadhi halali zipo.
(2) Walisema hazijasajiliwa kwa matumizi ya hapa nchini. Sisi tinajiuliza ni kwanini waliziruhusu ziuzwe madukani huko Dar pamoja na kiwandani Chemi Cotex? Huu ni uzushi mkubwa baada ya kugundua TAKUKURU imewabaini hila na uozo wao.
(3) Kutosajiliwa kwa jengo lile kwa kuifadhi vipodozi. Tunajiuliza ni kwanini walichelewa kutoa kibali licha ya malipo yote kufanyika?Kwa uonevu walilipeleka wizarani swala hili na kumpotosha waziri wa afya hivyo ikaamuliwa bidhaa zile ziteketezwe na BYC walipe 25% ya thamani yake.
Kwa waraka huu sisi wafanyabiashara wa vipodozi Arusha tunalaani kabisa tabia hizi za ya TFDA za kutuonea na tunaiomba serikali itusaidie katika haya:
(1)Tunaishukuru sana TAKUKURU Arusha kwa hatua stahiki ilizochukua katika sakata hili na tunaiomba ifatilie uozo huu na pia iwachukulie hatua kali wafanyakazi wasio waaminifu wa TFDA waliopora mali ya BYC pamoja na Philemon cosmetics.
(2)Tunaunga mkono juhudi za mheshimiwa Rais za kuhimiza wafanyabiashara kulipa kodi, kufanya biashara halali na kuanzisha viwanda. Tunaamini sakata hili limetokea ili kuwarudisha nyuma BYC LTD ambao ni wawekezaji wazawa wasifungue kiwanda, ilhali walilipia usajili BRELA pamoja na kodi TRA na ada zote za TFDA. Huku ni kukinzana na kaulimbiu ya mh Rais na kunatukatisha tamaa na tunakuomba Mh Rais pamoja na Mawaziri mfatilie hili sakata kwa undani.
(3)Tunamuomba mh. Waziri wa Afya mh Ummy Mwalimu arejee upya rufaa iliyopelekwa kwake na wafanyibiashara hawa, kwani tunaamini waziri alipotoshwa na TFDA. Tunalaani na kupinga kabisa amri ya kuteketeza bidhaa hizi kwani hata Mkurugenzi wa TFDA taifa ndg Fimbo alivifanyia uchunguzi na kuthibitisha ni salama kwa binadamu na havina viambata vya sumu. Si halali kuteketeza mzigo wenye thamani ya Milion 58 wakati ni salama.
Mwisho kabisa tunaamini serikali yetu sikivu italifatilia sakata hili kwa undani na haki itatendeka. Bado tunaamini TFDA Arusha imehodhiwa na wachache wasio waaminifu, inatumika kuturudisha nyuma na kwa hali hii kuikosesha serikali mapato mengi.