Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 37,141
- 46,402
Nimsoma na nimesikia taarifa toka aliyekuwa akiisemea ACT katika mkutano wao jana na waandishi wa habari , kuhusiana na uamuzi wa Chama kumuondoa Mteuliwa wa Rais kama mwenyekiti wa chama chao.
Pamoja na taarifa hiyo kwa umma, msemaji aliweka wazi imani aliyoionesha Rais kwa wateuliwa wawili ambao ni wanachama wao inamaana kwamba Sasa chama chao kipo Tayari kushika dola.
Napenda kupingana na kauli hiyo ya utayari wa chama cha Act kwa kuangalia teuzi mbili tu. Sina uhakika kama mtoa taarifa alijiridhisha pasi na shaka yoyote kuwa teuzi mbili pekee ndiyo sababu kuu ya wao kuonekana tayari kushika dola. Ila kama bado ACT wanaamini kuwa wapo tayari kushika dola kwa kutegemea teuzi inamaana kwamba, bila teuzi hizo chama hakina uhalali wa kushika dola, na kama ikatokea wateuliwa hao wakatumbuliwa basi kitakuwa kimekosa sifa ya kushika dola.
Ninachokiona mimi kuhusiana na teuzi hizi, ni Rais kuona kuwa hao wanaweza kumsaidia katika kuwatumikia wananchi na nikatika dhana ya kujenga utaifa na kupeleka ujumbe kwamba despite our differences in political ideologies we can still work together as country men to reach a common goal.
Sina hakika kama chama kisicho na miaka mitano ya uhai wake, kina uwezo wa kuongoza Taifa kongwe kama letu, badala ya kujiona kuwa Tayari wamekuwa, hii iwe chachu ya kukua kisiasa.
Nawakaribisha ACT kuitafakari upya kauli yao kwani haiendani na ukweli halisi.