Mkuu inaonekana inakula sana.. Mie ninatumia voda unlimited ya wiki moja, nimetumia tethering baada ya masaa kama sita hivi imekuja msg inasema "umefikia kiwango cha 2048MB. Endelea kutumia kwa kasi ndogo hadi tarehe ya mwisho".. Ina maana imekula kitu cha nguvu..
Sasa imekuja issue nyingine ambayo ninataka kuwauliza Voda wanamaanisha nini wanavyosema Unlimited..?
Pia inategemea amedownload nini though kwa dakika tano 200MB ziishe na mitandao yenyewe ya tanzania ilivyokimeo kuweza kudownload mb zote hizo kwa dakika tano
Sababu kubwa ni kwamba simu ina speed kuliko modem.
Modem kibongo bongo nyingi speed zake ni 3.6mbps au 7.2mbps chache sana zinazidi hapo wakati simu nyingi ni 21mbps au 42mbps. Mitandao yetu mingi sasa hivi wana speed zinazidi 10mbps hivyo unapotumia kudownload kitu na simu kinakamilika upesi.
Mfano computer inaji update na update na update yenyewe ina ukubwa wa mb200. Kwa modem ya 3.6mbps max speed itachukua kama dk 8 kwa modem ya 7.2 itachukua kama dk 4 wakati simu itachukua chini ya hapo.
Sababu nyengine ni kwamba unapoconect na simu pc yako inaona ni wifi na wifi nyingi zinamaanisha unlimited. Kunakua kuna apps hazili internet ukiconect na modem sababu zinajua ni mobile data ila ukieka tethering zikiona ni wifi basi automatic zinakula data