Tetesi ina yote, ila kwa hilo nadiriki kuchagua la UKWELI, ninayemsemea ni huyu mwenye mabinti wawili, wanaishi Tanga, ni suala la tetesi tu, fuatilia hapa na utaujua ukweli,
Hivi ukiandikiwa '1990s huwa unaelea nini kichwani kwako! Unajua ninaposema enzi za huyu mwenye red namaanisha kipindi gani
Mkuu TONGONI!
Hizi picha ni za Hussein? Kama unataka kuiishinda tetesi weka picha ya huyu jamaa 'anayetetesiwa' na si kuweka picha za jamaa zake.
Waliocheza na Hussein timu ya Taifa nimpakanjiaaaaaaaa..,ila brother umetuuzia cd,mgunda na careca hawakuwahi kucheza na Tenga,wale ni wadogo sana hata kwa mkwasa
Hawa ni baadhi ya waliokutana na HUSSEIN RUGA MWAKURUZO timu ya Taifa....Mkuu Obi hizo picha ni za Hussein...moja yuko pekee yake na nyingine na family yake na hii hapa nimekuongeza wakati akiwa timu ya Taifa 1987....
Shaka yangu iko kwa mgunga na careca zaidi,kwa kuwa wakati hao wakicheza pamoja na kina mkanwa makocha walikua kinanda na mziray ambao katika hali ya kawaida wakati tenga anacheza mziray sijui alikuwa malangali akisoma sekondari labda,hapo ndio kwenye tatizo,kuhusu makuruzo sifahamu sana kwa kuwa alicheza muda mrefu so inawezekana alicheza na tenga kidogo sina uhakika hapa,ila mgunda,mkanwa,careca,ali muamba,makene, n.k. kucheza na tenga hapana
Mengine yanaweza kuwa tetesi, Tenga unajua kacheza mpira na kina nani (sisemi enzike akichezea Kandambili au PA),
Nimesema enzi za kina Tenga, unajua Hussein kazaliwa 1950's umewahi kumskia mchezaji huyu?
Hussein ni mtu wa 60s na amemaliza Jumuiya Sec School 1981/1982
Kwenye hiyo picha nimwakumbuka wachezaji wetu wa 1980's mpaka 1990's waliotangulia mbele ya haki,niliowakumbuka ni marehemu michael kidulu,wa kati kati kabisa katika waliosimama,sahau kambi,kati ya hao makipa wawili waliopiga magoti yeye ni wa kushoto,kapteni wa timu ya taifa wakati huo Issa Athuman Mgaya wa kwanza kutoka kushoto walioketi.
Bwana Tongoni nahisi wewe ndio mhusika mkuu,tunashukuru kwa kujitokeza,vipi Hussein Marsha nasikia yupo huko uk pia,vipi unazo taarifa zake,amepotea sana shujaa wangu yule...tuna hamu ya kusikia kutoka kwake pia.
Kwanza nakutaka radhi nadiriki kukuita MUONGO ikiwezekana Mob ifuteni hii THREAD inachafua jina la mtu...kwanzA jina umekosea ni HUSSEIN RUGA MWAKURUZO na miaka mingi yuko UK na family ,mdogo wake ni ALLY RUGA MWAKURUZO yeye yuko NEDERLAND...na
HUSSEIN hakuwahi kucheza na TENGA.
Huyo ndo Mwakuruzo mwenyewe 'in side ten' wa Coastal Union mnataka nini tena !Mkuu TONGONI!
Hizi picha ni za Hussein? Kama unataka kuiishinda tetesi weka picha ya huyu jamaa 'anayetetesiwa' na si kuweka picha za jamaa zake.
Nafahamu kuwa huyu jamaa anayeitwa Hussein Mwakuruzo ni dereva wa daladala katika mji mmoja wa katikati ya Uingereza. Labda mleta habari ana maana Husein Makuruzo na sio Hussein Mwakuruzo, majina haya yanaonekana kuwa tofauti.
Sijamuelewa mwandishi labda tuibue mchango kwa kumkumbusha! ila mtu huyu binafsi kwa sasa sijui aliko japo jina lake na alichofanya katika soka hakijafutika kihivyo ukitaja Coastal Union!
kifupi kubishana hakutasaidia,mimi binafsi nimeonana nae jana na kikweli amechoka na ana uchungu kwani amekaa miaka 17 jela huko malawi baada ya kukamatwa na mzigo wa madawa ya kulevya,akitokea south africa,amechoka hata ukimuona utajua huyu amepigika but kulingana na maelezo yake leo atakua anaelekea Tanga.ki ukweli nimeongea nae mambo mengi sana tukiwa maeneo ya ferry na alikua anasema anarudi ubungo stand atalala pale ili leo watoto wake wawili na mkewe wataondoka Tanga kuja kumchukua kwa private car,ameniambia wameachiwa baada ya kugoma kula ndipo balozi mdogo wa Tanzania nchini Malawi ambaye amedai ni mzanzibar kuwatembelea gerezan baada ya mazungumzo siku iliyofuata wakapelekwa mahakaman wakaachiwa kutokana na vielelezo kutokuwepo,pia muda waliokua gerezan.hata hivyo mwezake alikufa wakiwa njia hivyo kuzikwa huko malawi.yey kaenda mpakani akadandia mafuso kuja bongo
Mkuu, ni ngumu kuielewa tetesi, Makuruzo kapotea miaka mingi, huyo Mwakuruzo anamjua Tongoni but Makuruzo mida hii anauingia mji alioupenda
Naunga mkono hoja ya kutaka kuwajua nguli wetu waliowika katika medani za soka miaka ya 80 na 1990
let us connect the dots..................
Mpakanjia alikuwa mfanya biashara na mkewe alikuwa mbunge...........
Endelezeni dots
Anaishi Mji wa Leicester,Uk na anaendesha mabasi ya Arriva.Mtoa habari amekusudia HUSSEIN RUGA MWAKURUZO ukitazama majina aliyo orozesha ya wachezaji waliocheza na huyo aliye muita HUSEIN MAKURUZO ni waliokuwa katika kikosi cha wakati wa MWAKURUZO na hakukuwa na mtu mwenye jina linalofanana na hilo