Tetesi:Hivi necta husahisha mitihani kwa mtindo huu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tetesi:Hivi necta husahisha mitihani kwa mtindo huu?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Kapo Jr, Jun 8, 2012.

 1. Kapo Jr

  Kapo Jr JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 60
  Wana jf mara nyingi nimesikia malalamiko kuhusu necta ktk usahishaji mitihani kiwango cha sekondari ngazi zote(o-level hadi advance),watahiniwa binafsi wanasahishiwa kwa kiwango cha kufaulu tofauti na watahiniwa walio mashuleni eti kwa sababu ma-pc wanafinywa ili waendelee ku-reseat mara kwa mara kwa maslahi ya wachache ili waendelee kulipia zaidi,naombeni ufafanuzi.nawasilisha
   
 2. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,793
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Hiyo ni kweli mkuu zamani wanafunzi wa private walikua na paper 2 au 3 kila somo wakati wa school wanafanya 1 au 2.siku hizi grade A ya school inakua 71%ilhali wa private 81% utashangaa anakandamizwa zaidi
   
 3. Mkomamanga

  Mkomamanga JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 818
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Mi sidhani kama kuna ukweli katika 'grading' maana cheti ukiona cha 'private candidates' na 'school candidates' vyeti vyao havina tofauti kwa namna ya kutoa grades za A, B, C, D, F nk kwa O-Level na A, B, C, D, E, S na F kwa A-Level. Tofauti tu nadhani ni kwa vile watahiniwa wasiokuwa mashuleni hawapati alama za kidato cha pili hivo wanafanya ile inayoitwa QT, na kuanzia miaka ya 71 taarifa za maendeleo ya mwanafunzi hazina mchango wowote kwa matokeo ya mwanafunzi.
   
 4. Pendael laizer

  Pendael laizer JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 961
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Necta baraza lote lifumuliwe manake ukiangalia wanaorisit ni idadi kubwa sana na wanaopata ni 10 ndani ya 100 au hata 9. Sasa siyo kweli kuwa hawasomi ila ni biashara iliyoko hapo necta na inafanywa na hao katika hilo baraza.
   
 5. m

  mzee wandimu JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2012
  Joined: Sep 23, 2011
  Messages: 441
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  hakuna kitu kama hicho mkuu acha kudanganya watu! grade za school na private ni sawa! sema nyie mnaoreseat huwa hamkomai mkifeli mnasingizia eti mmepandishiwa grading!
   
 6. mansakankanmusa

  mansakankanmusa JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,093
  Likes Received: 603
  Trophy Points: 280
  fanyeni utafiti, acheni upuuzi wenu, nawashangaa wanaopinga pia waislam wanaonewa,mimi sio muislam lakini islamic knowledge ni jiwe, wanaopinga wafanye utafiti, wenzetu weupe wanafanya tafit tena kama ni ishu inayohusu maumivu katika imani ya mtu hawafanyi masihala, vita Tanzania kama kule nigeria na liberia inanukia. kisa nyinyi mnaochonga bila tafiti, ni ubishi ubishi tu.
   
 7. Kapo Jr

  Kapo Jr JF-Expert Member

  #7
  Jun 9, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 60
  Yawezekana kweli ni biashara kwa wanaore-seat ndo wanaofaulu huwa wachache si kwamba hawana uwezo,necta wamewekeza
   
 8. R

  Rucha B. Rucha New Member

  #8
  Jun 9, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yawezekana ni ukweli wanabaniwa wazidi kuchangia mfuko wa elimu unajuaa kibongo bongo badget haitoshi kila mwaka, lakini cha kuwashauli hao reseater waendelee kukaza buti huku wakiamini balaza litabana na mwisho wataachia.. kwani kama ipo, ipo tu haina mashindano....!
   
 9. Kapo Jr

  Kapo Jr JF-Expert Member

  #9
  Jun 9, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 60
  Wenye ukweni shusheni hapa jf tuache kulea jipu laweza lipuka,baraza mbona wanatenganisha paper wakati wanaoreaseat wengi wameongoza paper mbele ya school candidates baada ya necta2 hufeli,siri kwa manufaa yao au wananchi?
   
 10. L

  Likavenga Member

  #10
  Jun 10, 2012
  Joined: May 27, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Wewe ni Bongolala kama jina lako,acha kupotosha umma.
   
 11. L

  Likavenga Member

  #11
  Jun 10, 2012
  Joined: May 27, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Hamna kumtafuta mchawi,Private Candidates wengi wao ni vilaza.Walishindwa wakati wako shuleni na walimu full time alaf unategemea wafanye maajabu mtaani kwa kujisomea vichochoroni na vichwa vimeshaingia moshi ? Alama wanazopata ndizo wanazostahili wewe kama ulifeli ni ubongolala wako tu.
   
 12. NingaR

  NingaR JF-Expert Member

  #12
  Jun 10, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 2,836
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  UKO SAHIHI MKUU.
  WAJINGA ni CHAKULA YA WASOMI
   
 13. Sunshow

  Sunshow JF-Expert Member

  #13
  Jun 10, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 943
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kuna umuhimu wa baraza kuwekwa kitimoto watueleze maana haliingii akilini private candidate wengi hupata alama za chini kulinganisha na walizopata wakiwa school candidate.
   
Loading...