Tetemeko la ardhi limetokea Kisanga mkoani Morogoro

Tetemeko la ardhi limetokea Kisanga mkoani Morogoro

Anotherperson

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2014
Posts
615
Reaction score
701
Tetemeko la ardhi limetokea huko Kasanga mkoa wa Morogoro Jumamosi hii ya tarehe 3 Machi mida ya asubuhi.

Kwa mujibu wa USGS feed tetemeko lina ukubwa wa magnitude 4.7 likionyeshwa kwa kidoti kikubwa chekundu tofauti na matetemeko madogo kuashiria lipo level kubwa.

Baadhi wamesikia vitanda vyao vikitingishika kabisa, mliopo Kisanga na maeneo ya mkoa wa Morogoro mnaweza kutujuza zaidi.

Kisanga.png

​
Source: 4.7 magnitude earthquake near Kisanga, Morogoro, Tanzania and Dar es Salaam, Tanzania : March 03, 2018 04:40
 
Nadhani hao USGS waje na taarifa kamili, kabla ya watu wa Kasanga.
Hawa wako na live update kwenye website yao ya matetemeko yote yanayotokea duniani ikionyesha location, magnitude na depth pekee mkuu
 
Hakuna tetemeko lisilotingisha vitanda, kwa tunaoishi maeneo ya matetemeko ni kitu cha kawaida, kipimo cha tetemeko ni athari zinazoonekana baadae.
 
habari za asubuhi wadau

leo asubuhi kulitokea tetemeko la ardhi Morogoro ila halikuwa na madhara zaidi ya kupita zake kwa mikwara mingi, ilikuwa majira ya saa moja dakika arobaini hivi.
 
Dah nilikuwa bado nipo nitandan gafla nikaona nyumba inatetemeka nilishtuka sana ....nilipotoka nje nikawakuta watu wanasema ilo ni tetemeko la ardhi,....limekaa kama dkka3 hivi ...
 
Back
Top Bottom