Rweye
JF-Expert Member
- Mar 16, 2011
- 17,034
- 7,590
Kwanza niwapongeze sana wenzetu wa FAO kwa kuamua kusaidia kurejesha hari ya chakula na kilimo kwa maeneo yaliyoathirika na tetemeko mkoani Kagera. Tunasema asante kwasababu kusema kweli ni kitambo hawa watu walihitaji msaada na hasa kutoka kwa Serikali lakini hawakuwahi kusaidiwa. Wananchi walilia njaa kwa kukosa chakula na bado Serikali haikuja na mkakati wowote wa dharura. Wananchi walilia wasaidiwe vifaa vya ujenzi kama saruji, mabati na nondo kwa bei nafuu lakini serikali ikawaambia wajenge viwanda vyao. Waliomba wasaidiwe wapatiwe michango ya rambi rambi lakini serikali ikawaambia michango ile haikuwa ya kwao, bali ni kwa ajiri ya kujengea miundombinu. Kiujumla hawa wananchi walitelekezwa na Serikali yao.
Sasa leo Mungu kawaona watu wake, shirika la FAO limewaona na limeamua kuwabeba. Kwa huo msaada uliotolewa wa miaka miwili katika kusaidia shughuri za kilimo na upatikanaji wa chakula si tu itawafuta machozi wahanga, bali pia itawapunguzia unyonge na upweke walioachiwa na Serikali yao. Na naelewa haya hayajaja ghafla tu, naomba tutambue kazi kubwa iliyofanywa na Mama Tibaijuka na Wanakagera wa ndani na nje kwa ujumla katika kutafuta msaada kutoka nje kwa ajiri ya kutatua athari za tetemeko. Tunawashukuru pia kikundi cha Face Bukoba kwa juhudi zao walizozionesha mpaka sasa. Mungu awatie nguvu na awaongoze.
Mwisho nimalizie kwa kusema, Serikali ipo kikatiba na kusaidia watu wake ni wajibu kikatiba. Ifahamike hata ikipita miaka mingapi, bado Serikali itabaki na hili deni kwa wana Kagera. Mashirika na makundi watafanya yao lakini deni la Serikali kwa huu mkoa halitaisha kamwe. Ni jukumu la wananchi kuona ni namna gani wanailazimisha Serikali kuwajibika kwao, kwa njia za kisheria ama kwa misingi ya kisiasa.