Tengeneza Urafiki na watu wanaofanya biashara unayoifanya au utakayotaka kuifanya "utafanikiwa"

Somo zuri. Naanza kulifanyia kazi very soon.
 

Mkuu umeeleweka vizuri sana, shukrani kwa nondo hii adhimu.
 
Uzuri wa teknolojia saivi kuna magroup ya whatsapp unakuta wafanyabiashara mnajumuika kwa pamoja
kwenye magroup kule kupotezana kwingi maana kuna wafanyabiashara serious na wasio

kwenye magroup ukiwasha data zinamiminika msg 700+ n ngumu sana kupata mentor pale

mbinu bora ni ya Man to Man unatafuta mtu wako unaeona anafanya unachofanya au unachotaka kukifanya

kisha unamvaaa taratbu hatua kwa hatua hadi mnakua marafiki,hata ikibd kwakununua bidhaa zake mara kwa mara

maana wafanyabiashara wengi n wachoyo wa kushea INFO ila njia pekee yakulegeza moyo wa aina hii ya wafanyabiashara

ni kuwaungisha bidhaa wanazouza,huwa naamini hakuna taarifa nzuri inayopatkana bila gharama hata ktk hili

watu wanatakiwa wawe tayari kutumia gharama ku win mioyo ya hawa wafanyabiashara wachoyo,si rahisi ila penye nia pana njia...
 
uzi mkali sana huu,
 

Ulicho post kina ukweli ila unfortunately HAKUNA narudia tena HAKUNA mtu atakuambia siri ya mafanikio ya biashara yake na wapi anapata stock kwa bei rahisi.

Kama ushawahi deal na biashara za china utanielewa....raia wenyewe mnaongea vizuri mkifika kule watu wanaku kataa wanaenda kwa chimbo lao wenyewe labda muwe mmeshibana sana na chances ni ndugu yako.....

HAKUNA mtu atakuambia biashara yake ana run vp mpaka anatoboa NEVER....ushirika wa hivyo unafanya kazi pale tu ambapo labda wewe umepata mteja kwenye biashara yako na wewe huna hyo bidhaa / service unampelekea mteja mwenzako ili akauziwe kdgo upate genj lako kwa juu au commission swala la kutaka kujua hadi undani wa mtu ujue hadi profits zake anapata vp. Ushirika huo HAKUNA labda awe baba yako.

Zipo communities za wafanya biashara wa aina flani ambazo huwa wanakaa pamoja kwa lengo la kupanga na ku influence market prices ili wote wasimame au wafanikiwe ila still inawezekana ila i’d say 50 % - 60% ila sio kila kitu utaambiwa labda uwe mamba haswa na wewe kwenye kutafuta ndio utajua ABC’s zote na hapo ushasota sanaa.

Watu wanafki sanaa biashara zina mambo mengi mnooo amini Muombe sana Mungu akuinulie mtu aje akushike mkono akuonyeshe game linachezwa vp watu wa aina hii wapo ila ndio hadi ubahatike. Kupata details za biashara flan cheza na watu flani flani wapambe (jifunze kuwa na jicho la kujua nani atakupa info unayoitafuta) watie helaa kama ni bata watie bata refu wanafunguka kila kitu ila sio matajiri wenzio. HAWAKUAMBIII !!!
 
Nimepigwa na kitu kizito katika Biashara sitakuja kusahau. Kwakifupi biashara ni usimamie wewe mwenyewe lakini ukisema akusaidie mtu ndani ya mwezi tu kwisha habari yako.
 
Nimepigwa na kitu kizito katika Biashara sitakuja kusahau. Kwakifupi biashara ni usimamie wewe mwenyewe lakini ukisema akusaidie mtu ndani ya mwezi tu kwisha habari yako.
Jifunze namna ya kumanage business, unaupungufu wa uelewa (sorry). Kwny hili eneo.
 
Umenena mkuu wabongo wachoyo sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…