TENDWA atatendwa tu...

john billy tendwa,msajili wa vyama vya siasa nchini,amegeuka mwanasiasa wa chama cha mapinduzi. Lakini,ipo siku atagundua kuwa ccm si chama cha siasa ili ni genge la waropokaji na wachumia tumbo. Watamtenda tu...
ni genge la wanyang'anyi!.
 
nchi hii ina vituko vingi
msajili wa vyama vya siasa kuteulia na raisi wa chama tawala,
polisi wana mamlaka ya kuzitisha maandamano halali au kuzuia bila kibali cha mahakama
msajili wa vyama vya siasa ana mamlaka ya kufuta chama kwa maamuzi yake binafsi na kwa utashi wake
viongozi wa tume ya uchaguzi kuchaguliwa na rais wa chama tawala
HAKI IKO WAPI TUSIKUBALI KUINGIA UCHAGUZI MPYA BILA HAYA YOTE KUBADILISHWA.

aiseee babaangu naunga mkono hoja
 
Tatizo hapa ni namna Tendwa alivyopata ajira. Haujawekwa utaratibu bora au wa kidemocrasia wa namna ya kumwajiri msajili wa vyama. Yeye ameajiriwa na serikali ya CCM na kaapa kwa Rais aliyeunda serikali ya CCM. Uteuzi au ajira yake si kama ya Jaji wa mahakama. His is very disposable! Hakuna utaratibu wa kumlinda kwa aliyempa ajira asimwachishe kazi kwa maslahi ya mwajiri. Anaweza kufukukuzwa kazi wakati wowote ule na wa kumfukuza kazi yeye mwenyewe anamjuwa. Hii inamfanya amwogope yule aliyemuweka pale. Hivyo katika hali fulanifulani lazima angalau aonekane kuwa anamtetea mwajiri wake. Na kwa sababu watanzania tumewekeza kwenye unafiki na ubinafsi na hasa unafiki basi Tendwa anajikuta busara zimemruka na kumtetea aliyemwajiri. Hii ni kwa sababu katika mizania yake anapima vitu viwili maslahi binafsi na maslahi ya umma. Kila mara anaona maslahi binafsi ni bora zaidi- kwani umma ni nani? Anajiuliza. Umma ni bora kuliko mimi na watoto wangu au familia yangu? Anajibu hapana! Ila kama kungekuwa na utaratibu mzuri wa kumpata msajili wa vyama pengine hayo yote yasingemkuta. Mfano Tendwa angeweza kuwa impartial kama kungekuwa Judicial Service Commission inafanya vetting,majina yanapelekwa kwa Rais halafu Rais anapeleka majina matatu Bungeni kupigiwa kura. Hii ingemfanya asiwe na sehemu ambayo angewajibika moja kwa moja. Bila hivyo tutaendelea kupiga kelele tu na hataweza kuwa neutral kwa sababu maslahi binafsi na ya yule aliyemwajiri yamewekwa mbele ya yale maslahi ya umma
 
John Billy Tendwa,Msajili wa Vyama vya Siasa nchini,amegeuka mwanasiasa wa chama cha Mapinduzi. Tendwa,mhitimu wa Shahada ya Kwanza ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,hatumii vyema uanasheria wake. Tendwa,aliyepata Uwakili tarehe 13/6/2008 na kuwa na nambari ya Uwakili 1018,hatumii weredi wake wa kisheria ipasavyo.Anajipendekeza kwa CCM na Serikali yake.

Zipo taarifa kuwa John Billy Tendwa anajiandaa kuwania Ubunge 2015 kwenye jimbo mojawapo mkoani Kilimanjaro. Ana matumaini kuwa atateuliwa na chama hiki cha kijani anachojipendekeza kwacho.Chama cha Mapinduzi hakijengwi wala kulindwa na Tendwa. Kilishajengwa na kulindwa na sasa kinateketea.Tendwa si msaada tena.

Kauli zake za kisiasa za kutishatisha vuguvugu la mbadiliko hazina nguvu.Hazina nafasi. Kwanza,hana mamlaka anayoyasema kwa namna anayojitambia. Chama maarufu kama CHADEMA hakifutwi hivihivi tu. Kama ni mpira wa miguu,basi refarii aumalize mpira huu akiwa tayari amejitafutia njia ya kukimbilia. Lakini,ipo siku atagundua kuwa CCM si chama cha siasa ili ni genge la waropokaji na wachumia tumbo. Watamtenda tu...

Katika maelezo yako yote nimevutiwa na hapo nilipo bold....Hii nchi kwa rushwa ni bab kubwa....Yaani mzee huyo hakuweza kuwa wakili miaka yote hiyo ndiyo kawa juzi na huko kwenye uwakili hakuna umri maalumu wa mtu kukoma kuwa wakili?

Kinachogomba hapo jamani si kitu kingine pension tu...Tusiporekebisha hapo utashangaa hadi watu wanaotakiwa kupumzika muda wao ukifika wanact as if they are in their 30s umri ambao ndiyo unatakiwa kuwa main actor kwenye nyanja zote za Taifa!
 
Tendwa ni Feki
John Billy Tendwa,Msajili wa Vyama vya Siasa nchini,amegeuka mwanasiasa wa chama cha Mapinduzi. Tendwa,mhitimu wa Shahada ya Kwanza ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,hatumii vyema uanasheria wake. Tendwa,aliyepata Uwakili tarehe 13/6/2008 na kuwa na nambari ya Uwakili 1018,hatumii weredi wake wa kisheria ipasavyo.Anajipendekeza kwa CCM na Serikali yake.

Zipo taarifa kuwa John Billy Tendwa anajiandaa kuwania Ubunge 2015 kwenye jimbo mojawapo mkoani Kilimanjaro. Ana matumaini kuwa atateuliwa na chama hiki cha kijani anachojipendekeza kwacho.Chama cha Mapinduzi hakijengwi wala kulindwa na Tendwa. Kilishajengwa na kulindwa na sasa kinateketea.Tendwa si msaada tena.

Kauli zake za kisiasa za kutishatisha vuguvugu la mbadiliko hazina nguvu.Hazina nafasi. Kwanza,hana mamlaka anayoyasema kwa namna anayojitambia. Chama maarufu kama CHADEMA hakifutwi hivihivi tu. Kama ni mpira wa miguu,basi refarii aumalize mpira huu akiwa tayari amejitafutia njia ya kukimbilia. Lakini,ipo siku atagundua kuwa CCM si chama cha siasa ili ni genge la waropokaji na wachumia tumbo. Watamtenda tu...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom