Tembo wavamia makazi ya watu -Kilimanjaro

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
TEMBO kutoka Hifadhi ya Taifa ya Tsavo ya nchini Kenya wamevamia makazi ya wakazi wa Kata ya Mengwe na kusababisha nyumba kadhaa kubomolewa na Tembo hao Inasemekana Tembo zaidi ya 30 walivamia kwenye makazi hayo na kubomoa nyumba ya mkazi mmoja wa eneo hilo.

Vilevile Tembo hao wameharibu nyumba na kuharibu hekta zipatazo 100 za mazao ya shambani kwa wakazi wa maeneo hayo na kusababisha hasara.

Tukio hilo lilitokea Mei 25 mwaka huu, katika kijiji cha Mengwechini wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, Naijaijai Koira alisema kuwa tembo hao huwa wana kawaida kuhama mbugani mwao na kusogea karibu na wakazi hao.

Amesema walipovamia katika makazi hayo walisababisha hasara ya kuharibu nyumba moja na nyingine zikiwa zimebomoka upande na kuharibu hekta na kuharibu mazao shambani.

Amesema toka kutokea kwa tukio hilo wakazi wa maeneo hayo wamekuwa na hofu kubwa hadi kupelekea kutembea kwa makundi kwenda kwenye shughuli zao na kurejea majumbani kwao kwa makundi.

Amesema wakazi hao wanajifungia ndani kwa muda mrefu na kusababisha shughuli zao za kila siku kutokwenda kama wanavyokuwa wanavyojipangia wenyewe na kuogopa kutembea kwa hofu ya wanyama hao.

Amesema kuwa Tembo hao huwa wanaonekanaga karibu na makazi hayo na imekuwa hawajawahi kufanya uharibifu mkubwa kama huu na wamekuwa hawafiki kabisa majumbani mwa watu ila walikuwa wanakaribia karibu na maeneo hayo na kuongeza hofu kwa wakazi hao.

Amesema wakiwaonaga tembo hao wanafika karibu na maeneo hayo askari wa wanyama pori kwa kushirikiana na wakazi wamekuwa wakiwauwa tembo hao kama njia ya kuwafukuza wasifike kwa wakazi hao.
 
Back
Top Bottom