Kwatozakuku
Member
- Oct 4, 2015
- 24
- 14
Katika Kijiji cha Mariwanda tarafa ya Mugeta wilaya Bunda jimbo la Bunda vijiji amboko kuna mradi wa serikali wa kilimo cha umwagiliaji cha mpunga kwa kutumia bwawa. Watu wengi sana wamehasika na kilimo hiki ambacho kwa kweli ni cha uhakika na kinalipa.
Shida kubwa inayowakabili wakulima ni tembo kutoka hifadhi ya Serengeti ambao huja mashambani na kula mazao. Mwezi wa kumi mwaka jana makundi makubwa ya tembo yalivamia mashamba ya mpunga na kuteketeza eka nyingi sana za mpungu. Kwa wakulima wengi tulipata hasira kiasi kwamba mitaji imekatika. Baada tukio hilo tulijaza fomu za madai kupia kwa ofisa kilimo lakini cha ajabu hadi sasa hutujui hatima yetu.
Tunaomba wizara husika ituangalie ili haki zipatikane.