Tembo 60 wateketezwa na majangili hivi karibuni

Yaani KINA---NA? Au mi sijaku-get?

HUYU KINANA KATIBU MKUU WA CCM TUSIPOKUWA MAKINI ANAWAMALIZA TEMBO WETU. tena wamempa rungu(ukatibu mkuu) hii inamrahisishia sana kusafirisha tembo..ukizingatia meli za kusafirishia anazo. KINANA p'se acha tembo wetu
 
Mkuu inauma sana.
 
Tanzania sees 'sharp rise' in killing of elephants.

Reports suggest the number of elephants killed has increased since the government suspended its anti-poaching operation after a month. http://www.bbc.co.uk/news/world-africa-25550722

Sixty elephants were "butchered" in November and December, compared with only two in October.

The security forces adopted a shoot-to-kill policy against poachers when the operation was in force in October.

The government suspended it after an inquiry reported human rights abuses.

( Photo courtesy of AFP)

http://www.facebook.com/photo.php?fbid=10153030867847588&set=a.384188547587.191382.59145437587&type=1&relevant_count=1
 



Maujia ya tembo yameongezeka nchini Tanzania tangia serikali ya nchi hiyo kusitisha Opereshieni tokomeza kutokana na kuwepo madai kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Naibu waziri wa Maliasili na utalii nchini Tanzania Lazaro Nyarandu amesema kuwa idadi ya tembo 60 wameuawa katika kipindi cha miezi miwili tu ya mwezi Novemba na Disemba ikilinganishwa na tembo wawili tu waliouawa mwezi mwa kumi mwaka huu

Hata hivyo idara za ulinzi zilikubaliana kuwaua majangili watakaobainika wakiwaua tembo hao kipindi ambacho msako huo ulikuwa ukiendelea mwezi Oktoba mwaka huu.

Hata hivyo serikali ilisitisha operesheni hiyo kufuatia malalamiko kwamba watekelezaji wa msako huo walikuwa wakikiuka haki za binadamu.

Waziri mkuu wa Tanzania alikaririwa akisema operesheni hiyo ilikuwa na nia njema lakini taarifa za kuwepo vitendo vya mauajia na ukikwaji wa haki za binadamu ndicho ambacho hakikubaliki na serikali.

Hata hivyo matokeo ya uchunguzi wa kamati maalumu kuhusiana na kuwepo kwa ukiukwaji wa haki za binadamu ndiyo uliosababisha Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete kuwafukuza kazi mawaziri ,Shamsi Vuai Nahodha wa jeshi la ulinzi, Emmanuel Nchimbi wa mambo ya ndani,waziri wa Utalii na maliasili Khamis Kagasheki na waziri wa Maendeleo ya Mifugo David Mathayo.

Nchi za kutoka bara la Asia ndizo zinazodaiwa kujihusisha Zaidi na biashara ya pembe za ndovu hali inayoongeza kasi ya ujangili na mauaji ya tembo nchini Tanzania.


bbc
 
Operesheni tokomeza ujangili inafanya kazi vizuri. Pinda alivyosema 'wapigwe tu' unadhani alikuwa na maana ya binadamu tu?????
 
TEMBO 60 wameuawa na majangili kwenye hifadhi mbalimbali nchini katika mwezi mmoja tangu operesheni tokomeza isitishwe.

Mauaji hayo yametajwa kufanyika katika Hifadhi za Selous, Rungwa, Burigi, Katavi na Ngorongoro.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alisema jana kwamba idadi hiyo ni sawa na wastani wa tembo wawili kila siku, inakwenda sanjari na kuuawa, kujeruhiwa kwa watumishi kadhaa wanaofanya kazi kwenye hifadhi. Alisema hayo Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna serikali ilivyojipanga kuhakikisha inatokomeza vitendo vya ujangili.

Source HabariLeo Magazine
 
Oparesheni tokomeza irudi haraka sana ili kuwanyoosha watu hawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…