Teknolojia yawatoa ushamba wabunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Teknolojia yawatoa ushamba wabunge

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Saint Ivuga, Apr 6, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Apr 6, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,515
  Likes Received: 19,934
  Trophy Points: 280
  Teknolojia yawatoa ushamba wabunge Send to a friend Tuesday, 05 April 2011 21:27 0diggsdigg

  Midraji Ibrahim na Israel Mgussi, Dodoma
  UTARATIBU mpya wa kufungua milango kwa kutumia teknolojia ya kadi maalumu katika majengo ya Bunge mjini hapa ulioanzishwa ili kuimarisha usalama umewababaisha wabunge wengi na waandishi wa habari.Kwa mujibu wa utaratibu huo ulioanza kutumika jana, kila anayeingia kwenye majengo yake hulazimika kutumia kadi maalumu kumwezesha kufungua mlango husika.

  Baadhi ya wabunge na mawaziri walionekana kuganda kwenye milango, baada ya kushindwa kuifungua na kulazimika kuomba msaada kutoka kwa wenzao.Kabla ya kikao cha kwanza cha Mkutano wa Tatu wa Bunge la 10 kuanza, Spika wa Bunge, Anne Makinda alisema matatizo yatakayotokea yanatokana na ugeni wa teknolojia hiyo huku akiwataka wabunge na waandishi wa habari kufuatilia kadi zao za kuwawezesha kuingia bungeni.

  Hata hivyo, baadhi ya waandishi wa habari walipewa kadi za wageni ambazo zilikuwa zinawawezesha kufungua mlango mmoja na hivyo kukwama walipojaribu kuingia milango ya ndani.Inadaiwa kuwa licha ya usalama, kadi hizo zitatumika kuratibu mahudhurio ya wabunge kwa sababu zitakuwa zikirekodiwa katika kompyuta kila anayeingia na kutoka. Ingawa lengo la Bunge ni kuimarisha usalama, baadhi ya wabunge, walionekana kutopenda utaratibu huo wakisema endapo kutatokea janga la moto hawataweza kukimbia na kupita milangoni mara moja.

  Wakati huohuo: Wakurugenzi katika halmashauri za wilaya nchini ambao kwa namna moja au nyingine wameonekana kuwa kikwazo kwa maendeleo ya elimu hasa ya sekondari watachukuliwa hatua.
  Akijibu maswali bungeni jana, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tamisemi (Elimu), Kassim Majaliwa alisema baadhi ya wakurugenzi walishindwa kusimamia vizuri fedha zilizotengwa katika wilaya zao kwa malengo ya kuchochea sekta ya elimu.

  Majaliwa alisema kwa kipindi hiki ambacho Serikali inaendelea kuwafuatilia wakurugenzi hao na kuchukua hatua dhidi yao, si dhambi kama wananchi wataendelea kuchangia nguvu zao kwa miradi ya maendeleo ya shule zinazopelekwa katika maeneo yao kwa lengo la kuziboresha.

  Alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu aliyetaka kujua kwa nini shule nyingi hazina madawati ilhali fedha zilizotengwa kwa ajili kuchochea maendeleo ya sekta ya elimu zilirejeshwa bila kutumika hadi Juni mwaka jana.

  Akifafanua swali lake la nyongeza, Lissu alisema taarifa ya Waziri Mkuu aliyoitoa bungeni mwaka jana ilionyesha Sh55 bilioni zilitengwa kuboresha sekta ya elimu lakini Sh21 bilioni hazikutumika hadi mwaka wa fedha ulipoisha na hivyo kurejeshwa. Swali hilo lilitokana na swali la msingi lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Kiambwa Mbaraka aliyetaka kujua mpango wa Serikali kuondoa kasoro mbalimbali zilizomo katika shule za sekondari za kata nchini.

  Akijibu swali hilo, Majaliwa alisema Serikali itahakikisha kuwa inakamilisha miundombinu ya shule ambayo bado katika kipindi pili cha utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES II).

  “Katika utekelezaji wa MMES II, kwa kipindi cha mwaka 2010 hadi 2014, Serikali itakarabati na kukamilisha shule za sekondari 1,800 kwa kuziwekea miundombinu yote muhimu, ikiwamo maabara, madarasa na nyumba za walimu,” alisema Majaliwa.Katika kutekeleza mpango huo wa MMES II, alisema shule zipatazo 500 zitagharimiwa na Benki ya Dunia ambayo imeridhia mkopo nafuu wa dola za Marekani 150 milioni, wakati shule 1,300 katika mradi huu zitagharimiwa na Serikali
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Apr 6, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,515
  Likes Received: 19,934
  Trophy Points: 280
  waongoza jahazi hawa
   
 3. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #3
  Apr 6, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Wengi wao nafikiri watakuwa wale wa CCM! Hivi hivyo vyumba vya bunge havina 'emergency exit' au 'fire exit' kweli? Kama milango ya dharura ipo basi hata hawaijui! Halafu hawa ndio tunataka watuwakilishe kwa makini kweli?
   
Loading...