Mimiwikolo
JF-Expert Member
- Mar 28, 2015
- 218
- 19
Wasiwasi ndio akili, wahenga walishasema hivyo. Nimekuwa nikisikia kuhusu goli la mkono la CCM na baadhi ya wadau kwenda mbali zaidi kwa kueleza nini kitafanyika. Moja ya vitu hivyo ambavyo vimenishtusha na kunipa wasiwasi ni "teknojia katika karatasi za kupigia kura".
Inasemekana zitatumika baadhi ya karatasi za kupigia kura ambazo ukipiga kura kwa mgombea tofauti na wa CCM basi ukishaikunja karatasi na kudumbukiza kwenye sanduku la karatasi za kura na kuja kuitoa baadae wakati wa kuhesabu kura ile "tick" inakuwa imehama na kuhamia kwa mgombea wa CCM. Hivyo itawafanya CCM washinde bila hata kutumia nguvu na inasemekana ndo maana JK anaponda starehe tu na wasanii kwani anajua ushindi ni wao. Huenda ikawa kweli au la kwani wahenga walisema tena kuwa lisemwalo lipo kama halipo basi laja... Wito wangu kwa intelligensia ya UKAWA/CHADEMA fanyeni haraka kufuatilia hilo kama bado hamjaanza kufuatilia isije ikawa balaa kama ni kweli. Pia nashauri kabla ya kuanza kutumika karatasi hizo, vyama vya siasa vishinikize kufanya sampling na kuzijaribu hizo karatasi kubaini kama kweli hilo lisemwalo ni halisi au la (nimewaza tu kwa sauti hapo coz mi sijui nini cha kufanya). Sijui kwa kweli nini wadau wa uchaguzi wafanye juu ya suala hili. Wasiwasi ndio akili. Mwelevu huwa hapuzii lolote lile lisemwalo kwani lisemwalo...