dawa yenu
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 2,829
- 3,733
Natamani nyakati zirudi nyuma. Turudi kule tulikotoka, turudi enzi za ujima! Turudi enzi za 1947. Globalization imenichosha, imenikinai bora turudi enzi zetu nafsi yangu itulie.Kwa takribani miezi miwili mfululizo nimekuwa nikifa kijerumani. Leo nimegoma, naivua tai shingoni na naipaza sauti yangu nyikani kila mwenye kusikia anisikie. Mwenzenu yamenifika shingoni, utandawazi sumu!
Yote haya yalianza pale nilipopata mpenzi mpya. Kama ujuavyo utamu wa penzi jipya hasa pale umpatapo yule aliyekidhi vigezo vyako. Kiukweli huyu baby wangu anajua nini maana ya huba, anajua kuniridhisha nami nikaridhika hakika ufundi wake kunako mahabati sijapata kushuhudia Afrika Mashariki na kati. Na kinachonisukuma zaidi kwake ni kwamba huyu laazizi wangu sisemi amekamilika bali ametimia. Anajua kubembeleza yaani kabla hajaanza kuongea nyoka ashatoka pangoni. Sifa zake hizo ndizo hasa zinanipa kichomi mwenzenu na hasa hii tabia yake ya kupenda social networks.
Yaani kutwa kucha mara kacomment, mara kapost mara kalike, asubuhi yupo facebook, jioni yupo instagram, mchana anashinda jamiiforums halafu anaibukia watsapp kisha anaingia tango halafu anarudi kwenye sms za kawaida, uuuuwwwiii!? Sasa huko kote mimi na yeye ni marafiki, naona anachokifanya. Kwenye magroup ya watsapp naona tu wanavyomuita inbox halafu yeye anakataa kiashuo yaani nguvu haitoshi kabisa.
Akiweka picha facebook utakuta likes mia tatu comments mia hamsini zinamsifia na kumchombeza kwa maneno matamu kweli kweli. Humu namo mara team bazazi imuite pm, halafu kwenye nyuzi zinazohusu dyudyu anashiriki kikamilifu yaani nateseka mimi. Mitandao ya kijamii imekuwa kero kwangu. Teknolojia imekuwa janga. Bora turudi enzi za barua, haki ya Mungu bora turudi enzi maana hamna namna.