TEHAMA TANZANIA (IT)

jikuTech

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2023
Posts
228
Reaction score
290
Nianze na Pale Mjini YouTube
Uki search " Jinsi ya kutengeneza Software " saaana inakuja Youtube Channel Ya NK -- NK- Computer Training,, kwa wingi sana, na Uki Muuliza ROBOT yoyote au wengine wanasema AI , wengine ChartGPT,,

Majibu unayo yapata huko mjini youtube na kwa ROBOT ni tofauti ambapo kwa utashi tu utaona kwenye ROBOT ndio kuna content za kueleweka ambazo ni tofauti kabisa na za kibongo kwenye youtube na sehemu zingine,

Najiuliza Ni lini Walianza kufundisha TEHAMA Kwenye Vyuo Tanzania, kama ni muda mrefu umepita,,,,,mbona wanataaluma kutoka nchi zingine wameweka content zinazotao mwelekeo na uhalisia wa jambo flani kwenye tehama , tofauti na urahisi walio uweka watengeneza content za TEHAMA wengi Tanzania ,,,

mwisho wa siku mtu hata ukiwa na ujuzi wako huo huenda bora kuliko watu wengine, usipo chukua muda wako kidogo kwenye maisha kutengeneza awareness ya kile unacho kijua. watu wengine hata wale unao wazidi taaluma wakitengeneza awareness wataonekana wana thamani sana kwenye hiyo taaluma kuliko wewe.

Sasa tatizo la wasomi wengi Tanzania ni Kulazimisha watu wawa thamani bila wao kutengeneza awareness

Kama haujui kutengeneza awareness na ni msomi huenda umewahi kusoma kwenye masomo yako na unapuuzia ,, Nita kuelekeza tena hapa Leo .
Ilii uweze kutengeneza awareness ni lazima utoe elimu kuhusu una jua kwa undani kiasi gani kwenye hiyo taaluma yako.

Binafsi mimi nawachukia sana baadhi ya wasomi wa Tanzania
Kwa sababu wamechagua au wanachoweza kufanya baadhi wengi ni kukosoa , Hata kama kosoa yao ni Ukweli na ni dhahili basi kosoa hizo zinakuwa hazina mvuto kutokana inakuwa haitofautiani na ya wengine ambao sio Wasomi wa Kiwango chao ,,,, kiasi ili ujue ni msomi mpaka akuambie mimi nina Degree, au A,,,B,,,,,C....


sasa ndugu zangu kwenye maarifa nadhani kuna kukalili na kuelewa kukalili athari zake hasi ndio hizo mpaka useme kwamba mimi nina Degree, au a b c ...... kusudi mtu akutazame kwa namna au hadhi unayo ona unayo.

Ambapo ni tofauti sana na kuelewa , Kuelewa ni kama Harufu huwa inatoka yenyewe kutoka kwenye chanzo ,yaani kama ipo lazima utajua tu harufu ipo , Mtu Ambaye amelewa maarifa au taaluma fulani ataonekana bila kushawishi watu ili wamuone na dhadhi iyo anayo itarajia.

Harufu ya mtu mwelewa wa taaluma fulani inaonekana kwa hoja zake tu. kuhusiana na hiyo taaluma.

Wasomi wengi wanashindwa kuteneza awareness kwa watu , wanabaki kulazimishia tu.
Mtu kama NK hadhira yake ina elewa kuhusu yeye , ipo aware ili uwashawishi kwenye kitu hicho ni lazima utoe Elimu yenye kiwango kamzidi NK
Lakini Ukienda kukosoa anacho kifundisha NK wakati yeye amefanikiwa kutengeneza awareness na wewe huenda ni msomi kumzidi NK na hauja tengeneza awareness kwa hadhira yoyote , yaani unakuwa una lazimishia tu.

Mfano : Msimsikilize huyo mimi nina Degree yeye ana Diploma .
au NK anafundisha vitu vidogo au NK haelewi

Pamoja na yote NK ni Mtanzania na nime Beza hapo juu content za Bongo nyingi ... Hapa kwanza niseme sija beza nime sema ukweli . Inabidi tu labda watu wanao elewa haya mambo wafanye vitu vya uhalisia ili kuleta wimbi lenye ushindani , watu wasiishie tu kuelekeza vitu vya mwanzoni,
Nisawa ukiwapa watu utangulizi wale wenye interest wata kufuata uwafundishe na hata ukiwapa kila kitu ulicho nacho mwisho wa siku na wao watakuwa kama wewe . Wakisha kuwa wameiva kutoka kwako watatoa Utangulizi tu , vingine wataficha ili kuvipata mpaka walipwe athari yake mwanafunzi anakuwa ndani ya Box, anakuwa anacho jua ndio hicho hocho.
Walimu wengi wanatoa utangulizi wa juu juu sana Huku wakiwa wanawazia Pesa ya Fasta Fasta.
Hali inayo pelekea connection inakuwa haipo kati ya wanafunzi wenye ujuzi wa mwalimu huyu na yule , wanabaki kutambiana na kila mtu kujiona bora kuliko mwenzie, Kila mtu anaficha anavyo ona vya thamani kwake kuvitoa mpaka alipwe.

Mbongo mara nyingi analipia kile anaona na anauhakika na matokeo yake , wanachukia ku take risk. ndio maana kuigana kwingi sana, kwenye majina ya biashara, biashara na sehemu nyingi

TEHAMA tanzania inakuwa kama makabila kila ilo lina utamaduni wake, wataaluma wa huku na huku. . Walio Hitimu TEHAMA bongo ni wengi sana Tangu wamefungua vyuo vya TEHAMA,

Baada ya hapo kila mtu anashughulika atengeneze Product yake ili apige pesa na bahati mbaya tehama inahitaji uwekezaji sana.
1. MUDA
- wakati wa kujifunza
-wakati wa kutengeneza
-Launching
zote hapo juu unakuwa hauja anza kupata hela kutoka kwenye jitihada zako.

2. MARKETING
kufanya marketing ya project yako inahitaji pesa , na Baada ya yote pesa inakosekana muda unakuwepo.
na mwingine pesa ipo ila hana uhakika kama wazo lake lita PAA

yote yote tunabaki na wataalamu wachache kwenye TEHAMA , na wengine hapo hapo wanachakugua kuwa matapeli , kwa maana kazi ndogo anataka pesa nyingi bila kujua mfululizo wa pesa ndio unaweza kumaliza shida au kupunguza shida na Sio ONE TIME inaisha tu kwani wangapi wamepata za hivi na hawana tena.
Wakati mwingine unaweza kuta kazi ni kubwa kweli ila anashindwa kumwelewesha mteja mchakato wa kazi. kwa sababu na yeye mwenyewe huyu mtaalamu amesahau pa kuanzia anakuwa anakumbuka pesa anayo lipwa na shida zake.

Nadhani wasomi katika TEHAMA waache maneno ya bila kutenda. maneno ya bila mikakati. Na kama wameshindwa wao wawasaidie wengine huenda hao wengine wakafanya kitu cha tofauti,


Binafsi nilipata interest na TEHAMA nikiwa na Miaka 14, Hapo lugha ya kiingereza ilikua tatizo kwangu , nikategemea sana content za Kiswahili cha tanzania kujifunza TEHAMA zilikuwepo za kuanzia,
Japo ilikua hata ukiingia Youtube ni chache sana zilikuwa hazina uzito na hadi sasa ni hivyo hivyo.

na waweka Content wengi walikua na mawazo kama niliyo kuwa nayo mimi , kupata Visitors katika Blogs zao, Followers kwenye Youtube kwa ajili ya Pesa za Matangazo , Huendana walikutana na uzio wa Watanzani kuto penda maarifa ya namna hiyo Saizi wale walio nifundisha hawapo tena. Hata niki GOOGLE.

Watanzania wengi hawapendi Long Terms wanapenda kufunika na kufunua wapate pesa .

Baadaye nikajua kiingereza nikapata maarifa mengi sana ya kuniinua na mpaka sasa mimi sija soma TEHAMA kwenye mfumo Rasmi .


Wasomi wengi ni Wazuri kwenye Mipango kuliko Kufanya. Mipango yenyewe inakuwa imeenda Shule
Jiunge nasi na uwe sehemu ya jumuiya kubwa ya wanafunzi na wakufunzi katika Tehama
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…