Tegeta Escrow imetuonesha bunge letu lina wabunge na viongozi wa aina gani

mfianchi

JF-Expert Member
Jul 1, 2009
9,720
2,000
Jamani kwa kweli hili sakata limetufumbua wengi,mimi asilani nilikuwa sijui aina ya wabunge na viongozi tulionao,na juzi ndio kwa mara ya kwanza nimesikia baadhi yao wakichangia ripoti ya tume,kusema ukweli kwa sampuli hii ya wabunge tulionao sidhani na siamini kabisa kama tunawezakulitegemea hili bunge hasa kwa wabunge wa chama tawala ambao ndio wengi.

Na nimeshtushwa na uzalendo walionao hao wabunge wa CCM kwa chama chao kuliko maslahi ya nchi ambayo yanawagusa wapiga kura zao.Pia ukiacha ushabiki hata uwezo wa kujenga hoja au kujua na kupima wanachoongea upo chini sana,nimeshangaa wabunge wa upinzani wameonyesha uwezo mkubwa wa kujenga hoja kuliko mipasho ya hawa wabunge wa CCM.Pia imenishangaza sana hata wabunge wasomi wa CCM wamegeuka mbumbumbu sijui dhamira zao haziwasuti.

Kwa mwelekeo huu tunapiga hatua mia nyuma na kwenda nusu hatua mbele,ni muda hao wabunge wangeanzia kupitia hansard kusikia yale wabunge wa zamani walivyokuwa wanawateteawananchi,akina mzee Tuntemeke Sanga,Kasaka,Kabuye,Nandonde,Ngalai.

Na katika maisha yangu sijawahi kusikia matusi bunge lilipokuwa na maspeaker kama Chifu Adam Sapi na Pius Msekwa,hata Mzee wa Viwango (wakati ule sio sasa)walikuwa kweli ma speaker,huyu wa sasa anavuna alichopanda kwa kifupi hana haiba wala uwezo wa kuwa speaker hata Zungu amemzidi kwa kiasi kikubwa,I wish Azzan Zungu angekuwa speaker kuliko huyu madame speaker,speaker gani anababaika kiasi hicho anashindwa kutumia kiti kutoa maamuzi yake?

Speaker gani anashindwa eti kujua jinsiya kuandika vizuri(kumpaka mafuta ya mgongo raisi)ili eti raisi asijue kama anamwingilia?je wakati wabunge wanapika kelele za wasurubiwe wasurubiwe akina Kagasheki,Nchimbi,Nahodha ,Ngereja je walikuwa hawaingilia mamlaka ya raisi?je huu si undumila kuwili wa bunge letu?kwanini wengine walazimishwe kujiuzuru na wengine waachiwe mpaka wapende wenyewe.
 

Tabby

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
10,593
2,000
Mimi nilichokiona kuhusu hili ni umuhimu wa kuweka viwango vya sifa ya mtu kugombea ubunge kwama angalau awe na elimu ya degree ya kwanza ya chuo kikuu. Hii itaondoa kuwa na kundi kubwa la wabunge, wanaogharimiwa fedha nyingi za taifa wakati hawana uwezo wa kutoa mchango bora kwa maendeleo ya nchi.

Tunahitaji kuweka sheria kwamba mgombea ubunge asiwe na historia katika kashfa ya ufisadi ama rushwa kwa kipindi kisichopungua miaka kumi kabla ya kugombea nafasi ya ubunge. Tutatengeneza bunge lenye watu wasioishi kwa ulaghai wizi, rushwa na ufisadi na kuondoa mwanya wa kusajili mafisadi bungeni wanaokwenda kule ili kulinda maslahi yao na ku influence maamuzi yaelekee matashi yao.

Sheria ya bunge iongeze vipengere vya ukomo wa ubunge, vijumuishe na ufisadi, ulaghai wa makusudi na kushindwa kutimiza majukumu yake kama mbunge ya ndani ya mikutano ya bunge na nje ya bunge. Wabunge wataacha kutumia mida kwa taarabu, vijembe na kitchen party ambayo hayana maslahi kwa wapiga kura wake wala taifa kwa ujumla.
Wagombea watakuwa makini na ahadi hewa za udanganyifu wanazotoa kuwahadaa wapiga kura, watalazimika kufanya kazi ili kutimiza malengo na wataishi kwa uadilifu kama viongozi wa jamii.

Wabunge wa kuteuliwa na viti maalumu wakome kuwepo kwa sababu hakuna wanayemwakilisha zaidi ya ushabiki wa vyama na kulinda uongozi uliowateua. Hatuhitaji watu wasiokuwa na mchango wa maendeleo bungeni na wanaokwenda kuongeza mob psychology ya kulinda watawala kwa gharama ya kodi zetu. Viongozi na watawala walindwe kwa ubora wa kazi zao na si propaganda na makelele ya ushabiki bungeni.

Sera ya 50% kwa 50% kati ya wanaume nawanawake kwenye masuala ya uongozi na utawala haina tija katika maendeleo. Itafika mahali watu watachukua nafasi ili kujaza hesabu wakati uwezo wao ni mdogo, tukawaacha watu wenye sifa na uwezo mkubwa kwa kutuletea maendeleo kwa ajili ya jinsia tu.

Kama ni wanawake ama wanaume kuongeza heasabu, watafute kwanza kukidhi vigezo na si kupewa kazi/nafasi kwa sababu ni jinsia fulani. Hapa tunacheza patapotea. Sote tumeona mambo yaliyoko bungeni. Tunahitaji watendaji na viongozi wenye sifa na uwezo wa kazi bila kuajli jinsia. Na wawajibike kwa mujibu wa katiba ya nchi.

Guys, to transform this community, tunahitaji kuwa real na serious!. Propaganda hazitusaidii.
 

Tabby

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
10,593
2,000
Na mawaziri wasiwe wabunge ili kuondoa conflict of interest wakiwa katika majukumu ya ubunge na kuisimamia serikali.

Na chama cha siasa, kitakachompitisha mgombea asiye na sifa zilizowekwa, kiwajibishwe kama chama na si kuwaachia wananchi waamue . Huu utakuwa ulaghai.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom