Unapohitaji matumizi ya solar power,lazima ujue pia matumizi yake na inavyofanyakazi. Solar panel kazi yake huwa ni ku-charge betri. Na solar panels zinatofautiana ukubwa kulingana na mahitaji ya mtumiaji.
Unavyoona panel imefungwa juu,huwa inafungwa kwa ufundi ili kupata makali ya jua muda wote,iwe asbh,mchana na jioni. Hapo inafanyakazi ya kuchuja umeme wa jua na kuchajisha betri km zile za gari. Km zilivyo betri za gari,zote zinakuwa na voltage 12. Huo ni umeme mdogo sana..ni sawa na betri za kawaida 8.
Kinachofanyika,mtumiaji inabidi awe na kifaa kinachoitwa inveter hiki ndo kinachukua umeme mdogo wa kwenye betri na kisha kuubadili na kuwa umeme mkubwa wa voltage 240. Ni km tu autonator kwenye gari inavyofanyakazi.
Kwa hiyo unaponunua panel,nunua pia betri kubwa. Mfano una panel ya wats 30,nunua betri ya N150. Nunua pia inveter ya wats 500. Na uwe na charger control. Maelezo ni mengi na me nasinzia,ngoja nilale ntarudi!!!