TEAM MEMBE haina Media Strategy?

TEAM MEMBE haina Media Strategy?

Hivi mbona sioni team membe wakifanya juhudi kwenye propaganda au ndio washakubali matokeo?
Membe ni mjanja Si unajua ni jasusi aliebobea yule,anafahamu now ni muda wa kujenga ushawishi kwa wajumbe wa vikao vya maamuzi hasa kamati kuu sio wananchi,maana Jina linaweza lisifike kwa wananchi,pia hataki kurudia makosa yaliyowafanya wakafungiwa na kuwekwa chini ya uangalizi kama mwenzake anavyorudia kufanya makosa ya kiufundi yatakayomcost,membe anafahamu jinsi mzee mangula alivyo mtu wa principle na makini,Si mlisikia lowassa alimtaja mzee mangula baada ya kung'atwa sikio kwamba ajaribu kuyazuia mafuriko aliyoyatengeneza cuz mangula is watching him
 
Wahenga walipata kunena kwamba KIMYA KINGI, HUWA KINA MSHINDO MKUU.....Watanzania makini hawapaswi kuhangaishwa na mtu mwenye uroho wa madaraka kiasi cha kutumia gharama kubwa kuyanunua madaraka bali tunatakiwa tutumie busara ndogo kujIuliza, je kwanini huyu mtu amekuwa na munkari na uongozi kiasi kwamba cha kuwa tayari kufanya lolote hata kama ni la kuvunja kanuni na taratibu za chama chake ili aupate uongozi..??,....Huruma hii kwa WATANZANIA wanaoshindia mlo mmoja ameitoa wapi....??...Kwanini anaonekana kuwa ni mwenye haraka na papara na uongozi....??....Nini kimejificha ndani ya dhamira yake juu ya taifa hili...??...WATANZANIA tuzifungue fikra zetu ili tuweze kuyachanganua mambo katika uhalisia wake....Tusizubaishwe na purukushani za wanasiasa walaghai...ule wakati tuliokuwa sote tukiusubiria kwa hamu na shauku hatimaye umewadia...tuliyavumilia mateso na manyanyaso kwa kipindi cha miaka mitano tukiamini kuwa siku moja yatakwisha...tukiamini kuwa hakuna marefu yasiyofika tamati...na hatimaye wakati umefika wa kufanya maamuzi sahihi ili yale mateso yaliyopita ya miaka mitano yawe historia...Hatupaswi kuyarudia makosa..Tukumbuke kuwa mustakabali wetu na watoto wetu kwa kipindi cha miaka mitano ijayo kinaanza na maamuzi ya leo.....Maamuzi yoyote mabovu yatapelekea majuto kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.....Tusisahau kuwa kiongozi makini hapimwi kwa sahani za pilau atakazo tugawia kipindi cha kampeni na wala si kwa vipande vya khanga wala fulana bali kwa sera zake makini na mipango inayotekelezeka....Tunapaswa kuchagua kiongozi ambaye hatatufanya tuyajutie maamuzi yetu huko mbele ya safari...tunapaswa kuchagua kiongozi au viongozi ambao tutajivunia kuwa nao kwenye safari yetu ya huko tunapopataka kwenda....Tunahitaji kiongozi au viongozi watakaotufanya tujutie kuwa ni kwanini hatukuwachagua mapema...Tunataka viongozi ambao watatusahaulisha mateso yaliopita na sio kutukumbusha mateso yaliyopita....Tunataka viongozi ambao hatutaona haya kuwakosoa pindi watakapo toka nje ya mstari....hatutaki viongozi waliojawa na viburi pindi waambiwapo ukweli au kukosolewa....Tunataka viongozi watakaolifanya taifa likimbie kimaendeleo na sio kuchechemea kimaendeleo.....Tunataka viongozi watakaotuunganisha WATANZANIA na sio kutugawa WATANZANIA.....Tunataka viongozi watakafanya maamuzi ya kitaifa kwa manufaa ya taifa na sio kwa manufaa ya familia zao na wapambe wao...Tunataka kiongozi mwenye uchungu na MATATIZO YETU na sio kiongozi atakayetumia matatizo yetu kama mtaji wa kujitajirisha yeye na vibaraka wake.....Tunahitaji kiongozi atakayetupa mikakati yenye kueleweka ya kulikwamua taifa letu.........lakini yote haya yanategemea sana maamuzi yetu ya leo........MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Myongeni mnyongeni haki yake mpeni. I personally not a fun of Edward. Lakini the guy is geneous. He knows what he wants. We all talk of Edward being Fisadi. But no body comes up with concrete evidence to indict him. Has he ever seen his day in Court? Of course not. My advice whoever wants to fight or deal with Edward afanye hivo kwa hoja. Siyo ujanja ujanja wa tuhuma ambazo siyo verifiable.
 
Masanja nimekukubali. Mtu anakuja hapa ooh lowassa ni fisadi ukimwambia tupe evidence hana. Lowassa amashatoa ruhusa kama unadoubt na utajiri wake nenda secretarieti ya maadili utapata taarifa kamili. Mnasubiria atakatwa kwenye cc. Mlikuja hapa mkasema atafukuzwa kwenye chama na kamati ya mangula anaendelea kupeta. Team maembe leteni concrete hoja sio uzushi tuu mmebaki kusubiri huruma ya kamati kuu
 
Membe ni JK type, hatuitaji aina ya watu kama yeye. Wenye unafiki, ambao katika hoja zote za ufisadi haonekani kukemea wahusika bali hutoa msimamo wa jumla tu. Hatuitaji Urais unaoanzia katika familia ya JK
 
Simba mwenda kimya....!. malizia!.

Pasco

Pasco:

Ni kweli unajua kutumia fahamu yako ya sita (6th sense). Ni watu wachache sana wamejaliwa fahamu hii. Kazi ya kum-groom ilipomalizika huko ndani aliletwa nje kuonyeshwa kwamba ndiye huyu. Lakini watu kwa sababu hawatumii hiyo fahamu hawajalibaini jambo hili. Juzi watu wawili seniour kabisa wameendelea kumuonyesha kuwa ndiye ajaye. Yule wa Zanzibar kamwambia yuko pamoja naye. Bwana mkubwa kasema kati ya Wizara ambazo hazijamsumbua kabisa basi ni Wizara anayoiongoza jamaa. Watanzania wanafafanisha kazi ya kuongoza nchi sawa na kazi ya kuwatongoza mabinti wa kizazi cha leo. Kwamba ukiwa mambo safi basi bila shaka wewe ndiye mwenye tiketi ya kuopoa.
 
Back
Top Bottom