Captain-Chui
Member
- Dec 11, 2014
- 80
- 49
TEAM Lowassa kweli mna nguvu kubwa kisiasa nchini, na mna wafuasi wengi. LAKINI msije mkajiachia hiyo nguvu yenu ikawalewesha mkafikiria mmeiweka CCM mfukoni. Pamoja na nguvu yake na marafiki zake na wafuasi wake mkumbuke LOWASSA sio CCM. Kwa sasa Team Lowassa bado mmelewa mnafikiri Lowassa ndio CCM. Walio nje ya Team Lowassa wameshaona dalili kwamba CCM haiwezi kumchagua Lowassa, na upinzani haitamkubali Lowassa.
USHAURI:
Team Lowassa fungueni macho muone dalili mpime mwelekeo wa upepo. Jiwekeni tayari kuweka mikakati ya kuhama CCM na kufungua chama kipya. Sasa hivi Team Lowassa mna nguvu ya kuleta mapinduzi ya kisiasa nchini kwa maana mna wafuasi wa kutosha. Jaribu kutafakari ushindani wa kisiasa utakavyokuwa mkali nchini kama kukiwa na Chama cha CCM, CHADEMA, na Chama cha TEAM LOWASSA, na vyama vingine. Huu ndio utakuwa mwanzo wa demokrasia ya kweli.