Zingatia hapa mkuu…………
Mke
anatakiwa kumheshimu mume wake, lakini heshima hiyo haimaanishi
kubeba maumivu ya kudumu, udhalilishaji, au kupoteza utu wake.
Mume anayestahili heshima ni yule anayejitahidi
kuwa na heshima, uwajibikaji, uadilifu na upendo.
Ikiwa kuna tabia kama ulevi uliokithiri, lugha za matusi, au kutowajibika kwa familia, ni haki ya mke kuweka mipaka na hata kusaka msaada kutoka kwa wazee wa familia, viongozi wa dini, au wataalamu wa ushauri wa ndoa.
Lakini asiache kuombea ndoa yake daima maana imeandikwa ….
(Mathayo 5:44):
“Lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi...”
- Mume au mke mwenye tabia mbaya anaweza kuombewa kila siku, lakini pia unachukua hatua za ushauri, mawasiliano, au hata kujitenga kwa muda kama kuna hatari.
- Hata unapoumizwa, haujibu kwa chuki, bali unachagua kutenda kwa hekima na utu.
- Unaweka mipaka bila kulipiza kisasi.