Inaendelea………………….
Enyi wanaume, wapendeni wake zenu, Hata wakikunyima password na uroda.
Kama huwezi kuvumilia PMS, mood swings, na maswali ya “Hivi unanipenda kweli?”,
kaa mbali na ndoa.
Kupenda mke si kama kulike picha zake tu, ni kuvumilia hadi kipindi cha “sijisikii kuongea” na “nimepika, lakini si kwa hasira.”
Maana nawaambia Kupenda ni sadaka ya nafsi, Yesu Kristo hakutupenda kwa sababu tulikuwa smart, alitupenda tukiwa na dhambi!
Kina baba, msiwachokoze watoto wenu, msifanye nyumbani pawe kama kambi ya mafunzo ya kijeshi.
Mzee unasema mtoto hataki kufanya kazi ya shamba, lakini wewe miaka 15 hujashika jembe!.
Usitegemee mtoto atafanya unachosema atafanya unachofanya. Watoto wa leo hawapigwi hadi wabadilike, wanapendwa hadi waone mfano.
Watoto, watiini wazazi wenu,hata kama wanachati kwa HERUFI KUBWA.
Kama mzazi wako haelewi Wi-Fi lakini alikulea na mshahara wa 120,000,
mheshimu. Wazazi ni Google ya kale,hawana graphics lakini wana wisdom ya kutosha kukuokoa. Usimdharau mama yako kwa sababu hajui VPN , yeye ndiye alikufundisha kutembea kabla hujafahamu Wi-Fi ni nini.
NAHITIMISHA
Kwa ufupi napenda kuwaasa yafuatayo;
- Ndoa si sherehe , ni sadaka ya maisha.
- Kataa ndoa kama hujaiva , lakini usiwachanganye walio tayari.
- Mapenzi bila maarifa ni kama gari bila brakes ,linapendeza kwa macho lakini ni hatari.
- Mungu ndiye mwanzilishi wa ndoa, si Instagram, si TikTok, si Netflix.
- Ukiolewa au kuoa bila kuwa na elimu hii , uko kwenye hatari ya kuoa kiwanja bila ramani,mwisho ukutwe umejenga kwenye eneo la makaburi kama isemavyo ramani ya mipango miji.
Na kwa wale mnaoendelea kusema "sitaki ndoa, nataka freedom", kumbukeni hata Yesu alijitoa kwa bibi arusi wake (Kanisa), hakuwa bachelor forever,hakuwahi kunyonga nyani kama nyie vijana wa hovyo.
- Chavalikungu