Team kataa Ndoa, nawaasa msikatae maarifa!

Team kataa Ndoa, nawaasa msikatae maarifa!

Paspii0

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2020
Posts
638
Reaction score
1,038
Napenda kuchukua dakika chache, kabla hamjaruka tena kwenda "self-care vacation" Zanzibar, kuwaeleza maneno machache yenye uzito wa mawe ya Mbudya kisiwani na utani wa nyanya wa Tandale.

Tumejua mnaendelea kukataa ndoa kwa visingizio vya;
  1. Wanaume wote ni mbwa 🙄
  2. Wanawake wa siku hizi wanapenda pochi sana kuliko mapenzi.
  3. Mimi ni single ila mingle.
  4. Nataka nipate PhD kwanza.
  5. Ndoa ni kifungo cha maisha.
  6. Mimi ni feminist,alpha lone wolf. A.K.A msimbe
Kwa heshima, kataa ndoa kama hujajiandaa , lakini usikatae hekima!.

Ndoa ni agano, si deal la Netflix la mwezi mmoja. Kuingia kwenye ndoa ukiwa na mtazamo wa "Try & Error" ni kama kuingia baharini ukiwa umevaa slippers.

Efeso 5:25 inasema “Enyi waume, wapendeni wake zenu kama Kristo alivyolipenda kanisa...”

Je wewe unaweza kufa kwa mtu unayemfollow Instagram au tik-tok tu?,Kama huwezi, usioe bado.

Kutoa mahari si kununua mke bali ni kuonyesha thamani.

Kama unaona mahari ni gharama, tafakari,Kwa nini unanunua iPhone 16 pro kwa milioni tatu lakini unasema mwanamke hapaswi kupewa ng'ombe wawili?
Thamani haipimwi kwa bei , lakini bei inaonyesha uamuzi wa moyo.
Kama huwezi toa ng’ombe, toa moyo wa kweli ,lakini usitoe ahadi kama siasa za uchaguzi.

Enyi Wake, watiini waume zenu ,lakini si kama mpo katika kambi ya Jeshi.

Kutii ni tunda la upendo , si kiapo cha mateka. Mungu hajasema mke awe remote controlled, bali awe msaidizi na si kama remote ya king’amuzi cha tv.
Mke si ‘second-class citizen,’ ni mshirika wa kwanza katika agano.

Itaedelea…………………….
 
Inaendelea………………….

Enyi wanaume, wapendeni wake zenu, Hata wakikunyima password na uroda.

Kama huwezi kuvumilia PMS, mood swings, na maswali ya “Hivi unanipenda kweli?”, kaa mbali na ndoa.
Kupenda mke si kama kulike picha zake tu, ni kuvumilia hadi kipindi cha “sijisikii kuongea” na “nimepika, lakini si kwa hasira.” Maana nawaambia Kupenda ni sadaka ya nafsi, Yesu Kristo hakutupenda kwa sababu tulikuwa smart, alitupenda tukiwa na dhambi!

Kina baba, msiwachokoze watoto wenu, msifanye nyumbani pawe kama kambi ya mafunzo ya kijeshi.
Mzee unasema mtoto hataki kufanya kazi ya shamba, lakini wewe miaka 15 hujashika jembe!.
Usitegemee mtoto atafanya unachosema atafanya unachofanya. Watoto wa leo hawapigwi hadi wabadilike, wanapendwa hadi waone mfano.

Watoto, watiini wazazi wenu,hata kama wanachati kwa HERUFI KUBWA.
Kama mzazi wako haelewi Wi-Fi lakini alikulea na mshahara wa 120,000, mheshimu. Wazazi ni Google ya kale,hawana graphics lakini wana wisdom ya kutosha kukuokoa. Usimdharau mama yako kwa sababu hajui VPN , yeye ndiye alikufundisha kutembea kabla hujafahamu Wi-Fi ni nini.

NAHITIMISHA
Kwa ufupi napenda kuwaasa yafuatayo;
  1. Ndoa si sherehe , ni sadaka ya maisha.
  2. Kataa ndoa kama hujaiva , lakini usiwachanganye walio tayari.
  3. Mapenzi bila maarifa ni kama gari bila brakes ,linapendeza kwa macho lakini ni hatari.
  4. Mungu ndiye mwanzilishi wa ndoa, si Instagram, si TikTok, si Netflix.
  5. Ukiolewa au kuoa bila kuwa na elimu hii , uko kwenye hatari ya kuoa kiwanja bila ramani,mwisho ukutwe umejenga kwenye eneo la makaburi kama isemavyo ramani ya mipango miji.

Na kwa wale mnaoendelea kusema "sitaki ndoa, nataka freedom", kumbukeni hata Yesu alijitoa kwa bibi arusi wake (Kanisa), hakuwa bachelor forever,hakuwahi kunyonga nyani kama nyie vijana wa hovyo.


- Chavalikungu
 
Kumpenda mtu, ni Miongoni mwa jambo la kipumbavu, Inafaa ujipende Binafsi 98% na 1% upende Vitu vingine, na kumpenda mtu mwingine kwa Uhusiano wa mapenzi 1%
kiongozi tambua,kumpenda mtu si ujinga, bali ni hekima ya kweli. Maandiko yanatufundisha wazi,

Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe’ (Mathayo 22:39).

Sio udhaifu, bali ni agizo kuu la kiroho na msingi wa ustaarabu wa kweli.Kumpenda mtu, hata yule asiyeonekana kuwa wa kupendwa, ni kuonyesha kwamba wewe mwenyewe una thamani ya ndani na moyo uliojaa huruma.
Mtu wa busara hupenda kwa akili, si kwa upofu. Hupenda kwa kusudi, si kwa hisia peke yake.
 
Mimi naomba kuuliza kwenye mke kumtii mume kuna baadhi ya wanaume kuhudumiwa familia ni kama wanaona wanatoa msaada pia wanakua na maneno ya kejelii na ya kuumiza sana kwa mke na kuna baadhi pia wanatabia za ulev uliokidhiri mpk kulala nje au kurud kesho pia anatakiwa kuheshimiwa na vile vile na ilihali yey mwenyew ajiheshimu? Ukimpuuzia na kumuanglia tu ni kosa?? Suala la mke kumuheshim mume mrekebishe kuwa kwa mume anayejiheshm na kuheshim familia yake..
 
mke kumtii mume kuna baadhi ya wanaume kuhudumiwa familia ni kama wanaona wanatoa msaada pia wanakua na maneno ya kejelii na ya kuumiza sana kwa mke na kuna baadhi pia wanatabia za ulev uliokidhiri mpk kulala nje au kurud kesho pia anatakiwa kuheshimiwa na vile vile na ilihali yey mwenyew ajiheshimu? Ukimpuuzia na kumuanglia tu ni kosa??
Zingatia hapa mkuu…………

Mke anatakiwa kumheshimu mume wake, lakini heshima hiyo haimaanishi kubeba maumivu ya kudumu, udhalilishaji, au kupoteza utu wake.
Mume anayestahili heshima ni yule anayejitahidi kuwa na heshima, uwajibikaji, uadilifu na upendo.
Ikiwa kuna tabia kama ulevi uliokithiri, lugha za matusi, au kutowajibika kwa familia, ni haki ya mke kuweka mipaka na hata kusaka msaada kutoka kwa wazee wa familia, viongozi wa dini, au wataalamu wa ushauri wa ndoa.


Lakini asiache kuombea ndoa yake daima maana imeandikwa ….

(Mathayo 5:44):“Lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi...”
  • Mume au mke mwenye tabia mbaya anaweza kuombewa kila siku, lakini pia unachukua hatua za ushauri, mawasiliano, au hata kujitenga kwa muda kama kuna hatari.
  • Hata unapoumizwa, haujibu kwa chuki, bali unachagua kutenda kwa hekima na utu.
  • Unaweka mipaka bila kulipiza kisasi.
 
Nimesikia mtu kalipa mahali ya ng'ombe 200. Yaani retirement plan unabadilisha kwa stress?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom