KaziIendelee
JF-Expert Member
- Oct 30, 2013
- 327
- 229
Kuhusu kuanzisha tozo la Tsh 20,000/= kwa kila Mwanafunzi wa Chuo Kikuu.
Serikali inapaswa kuingilia kati suala la tozo iliyoanzishwa na Tume ya vyuo vikuu nchini, kiasi cha Tsh 20,000/= kwa kila mwanafunzi nchini.
TCU imeanzisha tozo hili kwa wanafunzi Wa vyuo vikuu kinyume na regulation ya 14 (1) (d) ya "Universities (General) Regulations, G.N.No.226" ya mwaka 2013 ambayo inakitaka chuo kilipie "prescribed annual commission fee" kwa kila mwanafunzi aliyedahiliwa kwenye chuo husika. Jambo hili limepelekea wanafunzi kutoendelea kujisajili katika vyuo vikuu vingi nchini kwasababu tozo la TCU Tsh 20,000/= kwa kila mwanafunzi limeanzishwa bila kufuata utaratibu Wa kisheria.
Pia sheria ambayo TCU wameitumia, wameitafsiri vibaya kwa kuwataka wanafunzi walipe tozo hilo na isiwe chuo kama utaratibu ulivyokuwa kipindi cha nyuma.
Pia wanasheria tuwasaidie wanafunzi wanaoonewa nchini kwa kulazimishwa kulipa tozo hilo. Tusome "Regulation" ambayo TCU wameitumia katika Public Notice yao kupitia website yao Home - Tanzania Commission for Universities ili tuwasaidie wanafunzi na hata baadhi ya uongozi wa vyuo kupata tafsiri sahihi ya nani anapaswa kulipia hiyo pesa.
Pia Mhe. Rais JPM, suala hili linagusa tabaka ambalo ulikuwa unalilia sana liweze kutimiza ndoto zao za kielimu lakini usajili umeshasimama katika vyuo vingi nchini kwasababu wanafunzi wamekataa kulipa tozo hilo; ni wakati sasa, baada ya kulijua hili, pamoja na viongozi wengine MULITOLEE MAAMUZI, VIJANA TULIOWATUMA WAKASOME WANATESEKA MNO NA HILI SUALA. Kwani kwa namna nyingine lilipaswa kufahamiawa na bodi ya mikopo ili kiasi kitoke board halafu wanafunzi walipie, unfortunately haipo hivyo.
Serikali iingilie kati jambo hili ili lisije likasababisha mgogoro kati ya wanafunzi na uongozi Wa vyuo kuwa mkubwa nchini