Tcu na heslb wanawatakia nini watanzania. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tcu na heslb wanawatakia nini watanzania.

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by taffu69, May 24, 2012.

 1. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2012
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Nimekuwa nikifuatilia utaratibu unaotumiwa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) katika kudahili wanafunzi wanaotaka kujiunga na vyuo vya elimu ya juu na pia utaratibu unaotumiwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) kwa wanaoomba mikopo kwa ajili ya masomo kwa ngazi ya elimu ya juu ambao unatia shaka kwa kiasi kikubwa.

  Nakubaliana na ukweli kuwa kutokana na mabadiliko ya mifumo pamoja na kukua kwa teknolojia ya mawasiliano, ni vyema mambo mengi yakafanywa kwa kutumia teknolojia ya kisasa kama vile kudahili wanafunzi kwa kutumia mtandao wa internet na pia kutumia mfumo huo katika kuomba mikopo. Jambo linalotatiza ni kwa jinsi gani mfumo huo wa mawasiliano ulivyosambaa nchini na namna wale wanaotaka kudahiliwa wanaweza kupata huduma hiyo kwa muda unaotakiwa. Mathalani kijana ambaye yuko Nkasi, Ngara, Nanyumbu, Kibondo, Mugumu, Loliondo na kwingineko atakavyoweza kupata huduma ya mtandao wa internet akiwa kwenye maeneo hayo pasipo kulazimika kusafiri umbali mrefu kama sio kwenda Dar Es Salaam kufuata huduma hiyo tena kwa gharama kubwa.

  Mbali na hilo, hata mfumo wa kulipia ada stahili kwa ajili ya kupata fomu zinazotakiwa unatia mashaka na unaleta usumbufu mkubwa pia. Mfano, TCU wanataka kabla ya kufanya jambo lolote ulipe ada ya udahili kiasi cha shilingi 30,000 lakini ili uweze kulipa ada hiyo unalazimika kwenda kwenye tawi la benki ya NBC ili uweze kununua kadi itakayokuwezesha kujisajili kwenye mtandao wa taasisi hiyo. Nao HESLB wanataka kabla ya kupata fursa ya kuingia kwenye mtandao wao kwa ajili ya kupata fomu za mkopo ulipe ada ya shilingi 30,000 kupitia M-PESA.

  Hoja ninayotaka kutoa hapa ni kwa nini taasisi hizi zimekuwa na ufinyu wa kufikiri katika kupanga namna ya kushughulikia mambo haya kwa upana zaidi ikizingatiwa kuwa zinaendeshwa na watu wasomi na wanaojua mazingira halisi wanayoishi Watanzania. Mfano badala ya kulazimisha kufanya udahili kwa kupitia mtandao wa internet pekee wangetoa fursa kwa wale ambao hawana nafasi ya kupata mtandao wa internet kupata fomu hizo kwa ajili ya kuzijaza kama ilivyokuwa inafanyika awali. Aidha, mfumo wa kulipia ada stahili nao ungehuishwa kwa kutoa fursa ya kulipia kupitia mfumo ama taasisi nyingine badala ya kutegemea taasisi moja pekee. Mfano, benki ya NBC matawi yake yako mijini zaidi ukilinganisha na benki ya NMB ambayo matawi yake yamesambaa hadi vijijini hivyo ingekuwepo benki mbadala kwa ajili ya ya kufanya malipo ya ada husika. Hivyo hivyo kwa upande wa malipo yanayofanywa kupitia M-PESA ni wazi kuwa sio watu wote wamejisajili kupitia mfumo huo kwani kuna ambao wamejisajili kwenye TIGO PESA ama Airtel.

  Mbali na hayo, hata utaratibu wa urejeshaji wa fomu za mikopo unaleta usumbufu mkubwa kwani unalazimisha mwombaji kurejesha fomu kwa njia ya EMS pekee bila kujali mhusika yuko eneo gani. Mfano, kwa mwombaji ambaye yuko Dar Es Salaam angeweza kurejesha fomu hizo moja kwa moja kwenye ofisi za HESLB pasipo kuzituma kwa njia ya EMS ama kwa wale ambao wako mikoani na hawawezi kupata huduma hiyo kwa urahisi wangeweza pia kutumia njia ya posta.

  Ni vyema taasisi hizi zikaondokana na ukiritimba zinaoufanya kwa sasa kwani inaonesha wazi kuwa zinachangia katika kudumaza kasi ya ukuaji wa elimu na kupunguza ari ya vijana wetu katika kutafuta elimu. Aidha, ukiritimba huu unazifanya taasisi hizi kuonekana kufanya kazi kama mawakala wa makampuni/taasisi fulani kitu ambacho hakitoi picha nzuri kwa jamii ambayo kwayo taasisi hizi (TCU na HESLB) zinajiendesha kwa kutumia kodi ya Watanzania wote. Utaratibu unaotumiwa na taasisi hizi pia unaonekana kuwa unaleta ubaguzi kwani hauoneshi kuwajali watanzania wote kwa ujumla wao.
   
 2. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,029
  Likes Received: 3,052
  Trophy Points: 280
  Mie nilitegemea bunge liitume kamati yake kuchunguza ufirahuni huu unaofanywa na tcu na heslb mpaka kupelekea maenezi ya vvu kwa ndugu zetu hawa,wakishaugua ni nani atawatibia ama itakuwa hasara ya nani?
   
 3. MKL

  MKL Senior Member

  #3
  May 24, 2012
  Joined: Mar 2, 2012
  Messages: 126
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hakuna huduma itolewayo bure duniani hata kama inatolewa na serikali, maana kwa kulipa kodi peke yake inatosha kudai kuwa umelipia huduma husika ila kwa ishu ya TCU wazee fikirieni ikiwezekana mfumo huu wa kulipia 30,000 na unapewa nafasi ya kuomba kozi nane ufe ili kila mwombaji akanunue fomu chuoni ajaze kivyake na chuo husika ndio kimdahili, hapo hujahesabu nauli chakula na malazi bado photocopi za vyeti na ujinga mwingine mwiingi tulioupitia sisi tuliojidahili kwa njia ya fomu. Mfumo wa CAS umeweza kudahili watu kwa usawa kwani hata mwenye 30,000 tuu ataapply vyuo vingi hivyo kuongeza uwezekano wa kupata chuo tofauti na angenunua fomu moja kwa 30,000 chuo kimoja tuu kama ilivyokuwa hapo awali.

  Gazeti la Majira la leo tareh 24 linailaumu TCU kwa kudahili wanafunzi wengi wakati serikali inauwezo mdogo wa kuwalipia wote mkopo, hivyo wanashauri ni bora TCU ingedahili wachache ambao serikali inauwezo wa kuwapa mikopo woote, hamuoni kuwa huu ndio utakuwa ni UBAGIZI WA HALI YA JUU?
   
 4. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Kama kuna ambae anaona huu mfumo wa tcu wa kudahili wanafunzi haufai,bac ahame nchi.over
   
 5. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2012
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hapa sijaghusia suala la gharama ila utaratibu unaotumika na mazingira ya jumla ya nchi yetu.
   
 6. NingaR

  NingaR JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 2,836
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  TCU WAKO SAHIHI KABISA SEMA KUUZA VoCHa NBC NDO WALIKOSEA BOLA WANGE TUMIA NMB.
   
 7. b

  brian360 JF-Expert Member

  #7
  May 24, 2012
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 222
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Jamani namba za kumbukumbu za HESLB unazipataje?
   
 8. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #8
  May 24, 2012
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  watu wanaweza kuchangia 10m arusi moja...ila kuchagia elimu ya juu.. eti kila siku ni serikali tu!!!!
   
 9. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #9
  May 24, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Ile message ya m-pesa huwa inaanza na tarakimu 8 za kutambulisha muamala, ndio hizo.
   
 10. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #10
  May 24, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,947
  Likes Received: 1,272
  Trophy Points: 280
  wapunguze gharama. Acha ubabe
   
 11. Matope

  Matope JF-Expert Member

  #11
  May 24, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 539
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Sidhani kama ni mbayaa sana sema. Waalioko mbali na teknolojia hii nda wanapata tabu mfumo wa kulipia ilipaswa iwe Nmb then M-pesa,Tigo pesa,Airtel money na hata Easy pesa coz. Kila binadamu anaushabiki wake wao kama Tcu wangeweka mfumo wa kukubalianaa na malipo ya Makampuni yote haya note kama inatumika moja M-pesa means kuna ushabiki wa kibiashara ndani yake THANKS
   
Loading...