singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
KAMPUNI za Mawasiliano ya Simu za Mkononi zimepigwaa faini ya shilingi milioni 90 kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya kanuni za ubora wa huduma.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, jijini leo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Nchini (TCRA), Dk. Ally Simba amesema kuwa kampuni hizo zimepigwa faini tofauti kutokana na makosa mbalimbali ya utoaji huduma ya mawasiliano kwa wananchi.
Dk.Simba amesema kampuni ziliitwa na mamlaka ambapo zilikiri kufanya hivyo na kukubali na kosa na maamuzi yaliyofikiwa kuwapiga faini kwa mujibu wa sheria za nchi. Mkurugenzi Mkuu huyo alizitaja kampuni hizo na faini zake kuwa ni Airtel sh. milioni 22.5, Smart sh. milioni 12.5, Tigo sh. milioni 25, Vodacom sh. milioni 27.5 pamoja na Zantel sh. milioni 25.
Amesema kuwa kutokana kampuni hizo kushindwa kutimiza masharti TCRA itaendelea na utekelezaji wa sheria na maamuzi mengine kwao kwa mujibu wa sheria zilizowekwa.Amesema baadhi ya makosa ni simu iliyopiga kudai kuwa inatumika wakati sivyo, wakati mwingine simu unapiga mwito wake unadai simu hiyo haipatikani wakati simu hiyo iko hewani.
Aidha amesema kuwa watoa huduma wote wa simu za mkononi kuhakikisha kuwa huduma zinazotolewa na kuzingatia vigezo vilivyoanishwa. Dk. Simba amesema kuwa kampuni za simu za mikononi zimejikita katika kujitangaza kwa njia mbalimbali katika kuweza kupata wateja wapya lakini hazifanyi uwekezaji wa huduma bora kwa wananchi wanaotangazia.
Hata hivyo TCRA imeipiga faini kampuni ya Azam Marine sh. milioni 5/= kutokana na kufanya usafirishaji wa vifurushi kutoka Dar es Salaam na Zanzibar bila kuwa na leseni ya utoaji wa huduma hiyo. Amesema kuwa ni kosa kwa Azam Marine kufanya huduma ya posta bila kuwa leseni huku wakikri kufanya biashara ya kusafirisha vifurushi.
Kampuni ya Rifalo imepigwa faini sh.10 kutokana na kufanya masafa ya ujumbe mfupi bila kuwa na kibali cha TCRA na Rifalo ilikiri kufanya hivyo. Dk. Simba amesema kuwa walipewa namba mara ya kwanza kwa muda na baada ya kuisha hawakuweza kuendelea huku wakiendelea kutoa huduma ya ujumbe mfupi.