India wana mfumo mzuri sana. TCRA yao imepiga marufuku vifurushi vinavyouzwa na makampuni kama DSTV, Startimes, Azam etc kwa sababu mtu analazimishwa kulipia channels kibao na nyingine wala haangalii.
Wewe angalia kifurushi unacholipia sasa hivi kina channel hata 100 zinafika lakini unaangalia channel 10 au 15 tu. Unalazimika kulipia channels kibao nyingine za kichina au kihindi wala huangalii
India mteja/mtazamaji anachagua channels anazotaka yeye kuangalia tu na inakokotolewa bei ya channels hizo alizochagua. Kampuni kama DsTV hawaruhusiwi kuuza vifurushi walivyochagua wao
Ni mfumo mzuri huo. Kuliko sasa azam wamekuja watuharibia mfumo wetu wa zamani,unalipia hela ndefu,michanel yenyewe mibovu,hawana msimamo kwenye vipindi.
Humo utakutana chanel za wanyama tu ndio nzuri zingine zote chenga tu. Azam isinyeshe mvua kidogo tu imekata.
Nimemiss sana ungo mkubwa,humo Mozambique ndani,imo ya michezo,kuna chanel za ITV humo. ITV wana msimamo kwenye vipindi hawabadiri kipindi eti ksbb ccm wanahutubia mahala.
Humo wakirusha tamthilia inakuwa iko vizuri sana unaielewa,wamewahi kurusha kama acaprucobay,ilivutia sana.
Azam wanaipromot sultan,ya kiduanzi,sultan watu wenye uelewa wanauawa sultan anabakiwa na maronyoronya tu. Imepoteza mvuto kwa kasi tamthilia inaigizwa kama inarudi rivas.
Kuna ingine inayotangulia kabla ya sultan nayo kama imelewa hivi.
hili la ving'amuzi litakua trick muhimu sana kwenye uchaguzi mkuu ujao,, na watu mtakuja hapa kumshangilia kama mazwazwa,, ilihali leo wametia pamba masikioni,,
Ndio maana hawa mbwa mikoani wanapigwa na wahindi wa cable tv.
Wale jamaa ni poa sana aisee, mnapatana kwa mwezi ni elfu 20 mfano, unapigwa kachumbali iliyoenda shule,documental na burudani mixer habari, na cartoon. channel kali za mipira zinaachiwa siku kukiwa na mechi tu.
Kama unalipia channel 50 kwa 18,000 it means kila channel unalipia sh 360 so kwa hali hii unaweza lipia 5000 ukpata channel 20 unazogaka endapo kila channel inatofautiana bei
Hii ni point muhimu Sana! Hasa Dstv wanaboa sana kwakweli mtu unawekewa michanel ya kichina! Mara ya kinigeria ya lugha ya Yoruba au Hausa! Yaan mtu unalipia laki na kitu afu channel unazozipenda hazizid kumi!
Hayo makampuni ya ving'amuzi ni wezi tu, wa mikoani huku tuna huduma za cable tunaangalia machannel ya kibabe kama bein sport, espn, sports 24, discovery zote, national geographic zote, Sony zote kwa buku 15 tu.
Halafu hata ukipitisha miezi miwili bila kulipa hawakukatii huduma bali wanakubembeleze ujitahidi kulipa.