GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 63,611
- 127,998
Yaani kila Siku Wateja wa Simu za Mikononi tunapata usumbufu wa kupokea Meseji za usumbufu na kutapeliwa na Watu ambao kwa taarifa za chini chini kabisa zinasema kwamba wanashirikiana na Watendaji ( Wafanyakazi ) wa Makampuni ya Simu makubwa nchini Tanzania lakini nyie ( TCRA ) mpo kimya tu.
Hivi hii nguvu kubwa mliyoitumia kuwaita akina Diamond na Nandy kisha ' mkawabembeleza ' waombe radhi / msamaha mngeitumia kuwasaidia Watumiaji wa Simu msingefanya jambo la maana?
TCRA mnataka kutuambia kwamba mmeguswa sana na ' Upuuzi ' kama siyo ' Upumbavu ' wa akina Diamond na Nandy na kutusahau Sisi Wananchi wenu ambao kila uchao tu tunapokea meseji za Kuudhi kama siyo Kusumbuliwa na kuna Wenzetu pia wanaotapeliwa na si ajabu hata hivi sasa kuna Mtu ameshatapeliwa.
TCRA uweledi wenu hapa uko wapi? Je tukihisi kwamba labda mnashindwa kulifanyia hili Kazi pengine na nyie mna 10% zenu za huu Utapeli na mnafurahia jinsi Watumiaji wa Simu za mikononi tunavyosumbuliwa na mameseji ya hovyo hovyo tutakuwa tunakosea?
Halafu wenye ' akili ' tulidhani katika kuhakikisha kwamba tabia mbaya na matendo machafu yasiyo na Kinidhamu ya Wasanii Wetu yanakomeshwa basi ile jana pale pale mngewapeleka Polisi au hata Mahakamani kuwashtaki hao akina Diamond na Nandy ila cha kushangaza nimedokezwa na Mtu aliyekuwepo eneo la tukio ile jana kwamba nyie ( TCRA ) ndiyo mlikuwa mnawabembeleza akina Diamond na Nandy waombe msahama na naambiwa baada ya kumaliza tu ile Press Conference yao ' Wafanyakazi ' wenu walikuwa wanapigana ' vikumbo ' kupiga nao ' Selfies ' huku wengine wakinywa nao Chai.
TCRA badilikeni tafadhali kwani ' Utendaji ' wenu hauakisi uzuri wa Jengo lenu hilo, mahala lilipo na jinsi mnavyoonekana kupendeza na Suti zenu Kali na Magari yenu makali ya Kifahari mliyonayo.
Nawasilisha.