ng'adi lawi
JF-Expert Member
- Sep 27, 2014
- 2,956
- 1,114
Serikali inasisitiza wafanyabiashara wote watoe risiti za EFD wakati wanapouza bidhaa au huduma. Tunaponunua muda wa maongezi tunapata ujumbe unaoonyesha jumla ya pesa bila kuonyesha kodi ya VAT. Hivyo hatuna hakika kama kampuni za simu zinalipa hiyo kodi wanayokusanya kutoka kwetu. Nchi ndogo kama Mauritius wanayo mtambo huo. Waheshimiwa Mbarawa na Phillipo Mpango kazi kwenu.