Habari ya asubuhi!
Kuna 'website' inaitwa 'Hubpages' watu wengi wanapenda kuitumia kama 'alternative' ya 'blog'. Iko kama vile 'platform' ya 'blogger' lakini yenyewe haulipii 'domain' wala 'hosting'. Wao pia wanatumia mfumo wao wa "Google Adsense" ambayo ukiomba ndani ya masaa 24 unakubaliwa. Lakini huwezi kuitumia kwenye 'blog' nyingine tofauti na hii ya 'Hubpages'. Jinsi wanavyolipa kwa wastani ni 0.8$-2.5$ kwa kila 1000 'views'. Kinachofanyika ni kwamba, unaandika makala yoyote kwa lugha ya kiingereza kisha unai'publish' kwenye 'profile' yako. 'Moderators' watai'review' na kama umeiandika kwa mtiririko mzuri(kiingereza fasaha na inasomeka kwa urahisi) wataweka matangazo ya 'adsense'. Kazi ya ku'review' inafanyika ndani ya masaa matatu. Kama umeiandika vizuri, wataweka matangazo kwenye hiyo makala na pesa itaanza kusoma kwenye akaunti yako ya 'Google Adsense' kutokana na watu watakaoisoma makala yako. Vilevile kuna mfumo wa 'Amazon Affiliate' ambao unaweza kujiunga na kukubaliwa upesi tu kama huo wa 'Google Adsense.'
Nilijaribu kuitumia lakini nikubali tu kuwa kiingereza changu siyo kizuri, sikukidhi vigezo.
Kama unajiamini kuwa unaweza kuandika makala kwa kiingereza kinachoeleweka. Waweza jiunga na kuanza kupiga pesa.
Sina uhakika kama sheria ya TCRA inaweza kukufuata hadi huko. Tuseme, hiyo 'Hubpages' iko kama 'Jamiiforums' hivi. Kiasi kwamba, wewe mtumiaji wake hauimiliki. Hivyo 'issue' ya kuisajiri ili kupata leseni haiwezekani.
Nawasilishaaaa, wajuzi zaidi wanaweza kufafanua zaidi